WAKILI
mmoja wapo anayemtetea Elizabeth Michael Fulgence Massawe akimsalimia
' Lulu' kabbla Jaji Dk. Fauz Twaibu hajaingia Mahakamani jana asubuhi
katika Mahakama Kuu ambako kesi hiyo ilipigwa tena kalenda hadi Juni 25
mwaka huu. Pia Jaji Fauz amezitaka pande zote mbili yaani Wakili wa
Serikali pamoja na Jopo la Mawakili wanaomtetea kupeleka vuthibitisho
kuhusiana na umri wa Lulu Mahakamani hapo.
MAHAKAMA
Kuu kanda ya Dar es Salaam imewataka mawakili wa utetezi na jamhuri
kuwasilisha uthibitisho kuhusu umri wa msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’
kabla ya kutoa uamuzi wake Juni 25, 2012.
Agizo
la Mahakama hiyo lilitolewa jana na Jaji Dk. Fauz Twaib anayesikiliza
madai ya utata wa umri wa msanii huyo nyota wa maigizo nchini.
Kabla
ya kuahirisha kesi hiyo Jaji Dk. Twaib alizitaka pande mbili
zinazobishana kupeleka vithibitisho vya hati ya kiapo cha cheti cha
kuzaliwa ili kujiridhisha umri sahihi wa Lulu.
Kwa
upande wake wakili wa mshitakiwa Flugency Massawe alidai mahakamani
hapo kwamba hadi Juni 13 atakamilisha vithibitisho hivyo wakati wakili
wa serikali Elizabeth Kaganda alidai kazi hiyo ataikamilisha Juni 22
mwaka huu.
Lulu
anayetuhumiwa kwa mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba Aprili 7
mwaka huu anadaiwa kuwa chini ya miaka 18 huku jamhuri wakidai kwamba
mshtakiwa huyo ana zaidi ya umri huo.
No comments:
Post a Comment