MSANII mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Hamis Mwinjuma ‘Mwana
FA’, amesema kuwa ameshtushwa na habari chafu zinazoenezwa juu yake na
kuwataka Watanzania kuacha simulizi za kusadikika na kusimama katika
ukweli.
Hayo aliyasema katika mahojiano yake na kipindi cha Friday Night Live
(FNL), kinachorushwa na televisheni na Radio East Africa, kufuatia swali
aliloulizwa na mtangazaji wake Sam Misago juu ya tetesi kuwa yeye ni
muumini wa dini ya Freemason.
“Ifike kipindi Watanzania watambue kuwa si kila mafanikio miongoni
mwetu yataletwa na Freemason. Nazushiwa hilo kutokana na aina ya mvuto
wangu na kazi zangu, lakini kamwe siwezi kuwa muumini wa dini hiyo,”
alisisitiza FA.
Katika kipindi hicho, Mwana FA alitamba kuendelea kubaki juu katika
sanaa, kutokana na kufanya mambo kwa umakini, kunakotokana na kuumizwa
kichwa kabla ya kutoa singo mpya.
Alitumia fursa hiyo pia kutambulisha na kukitolea ufafanuzi kibao
chake kipya cha ‘Ameen’ alichoimba kwa kumshirikisha Dully Sykes.
mh''v'2 v'ngine hav'eleweki ukweli n upi uongo n'up? but kila m2 na iman yake''amini v'le wew unavyoamini;;kwani kivyovyote v'le wa2 hawaach kusema hata ufanye nn''watasema 2 kama c'o h'l' ba'c n' lile''Ila safar ye2 n moja'''haku& atakaekwepa'''nma kila m2 ataubeba mzingo wake mwenyewe'''
ReplyDelete