EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, June 13, 2012

‘Nusu ya wajawazito hufanyiwa upasuaji’


HUENDA wanawake wengi zaidi nchini wakapata ulemavu wa kudumu baada ya kubainika kuwa, wengi wao hujifungua kwa njia ya upasuaji. Uchunguzi uliofanywa nchini, umebaini kuwa idadi ya wanawake wanaojifungua kwa upasuaji inazidi kuongezeka siku hadi siku.  Imebainika kuwa nusu ya wanawake wanaojifungua katika hospitali hizo hufanyiwa upasuaji.

Takwimu zilizopatikana kutoka Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili zinaonyesha kuwa mwaka 2008/2009 wajawazito 4,250 sawa na asilimia 44.7 walijifungua kwa njia ya upasuaji na 2009/2010 wajawazito 4,490 sawa na asilimia 48.

Katika Hospitali ya Amana kwa siku moja madaktari huwafanyia upasuaji wajawazito 10 hadi 11na kati ya Julai mwaka jana hadi Mei mwaka huu, Hospitali ya Amana imefanya upasuaji kwa wajawazito 1,439.
Wakati takwimu hizo zikionyesha hivyo Amana,  katika Hospitali ya Temeke wajawazito 730 walifanyiwa upasuaji kwa mwaka jana pekee.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka katika hospitali hiyo, kwani kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu, wajawazito 12 hufanyiwa upasuaji kwa siku.Kama kasi hiyo ya upasuaji itaendelea hivyo, itafanya hospitali hiyo kuwa na idadi ya wanawake wajawazito 4,380 waliojifungua kwa upasuaji kwa mwaka huu.

Takwimu hizo zinaonyesha kuwa kati ya wajawazito wanaojifungua kwa upasuaji, asilimia 82 hutaka wenyewe kwa sababu zao binafsi, huku waliobaki wakilazimika kufanya hivyo kutokana na matatizo ya kiafya.
Sababu za upasuaji
Mwananchi Jumapili ilifanya mahojiano na wanawake kadhaa walijifungua kwa njia ya upasuaji, kati yao walikiri kufanyiwa upasuaji bila sababu za kitabibu ambazo ni  Kuchoshwa na ujauzito: Eugenia Mwaibabile, mkazi wa Keko jijini Dar es Salaam alisema alimuomba daktari amfanyie upasuaji kwa kuwa alichoka kukaa na mimba kwa muda mrefu.

“Nilichoka sana! Niliona siku zinapitiliza sioni dalili ya uchungu, nikaenda kumwambia daktari ni bora anifanyie upasuaji,” alisema Eugenia. Eugenia alisema baada ya kumwambia hivyo, daktari wake hakumuuliza maswali mengi zaidi, baada ya saa chache, aliingizwa chumba cha upasuaji.Wanaogopa uchungu: Anamaria Mwendapole, yeye alikiri kuwa aliogopa kupata uchungu wa leba, hasa baada ya kusimuliwa na rafiki zake.

“Sikutaka kupata uchungu, nilimwambia daktari wangu mapema kwamba siku zikitimia nakuja, nafanyiwa upasuaji,” alisema.   Kuharibu maumbile: Baadhi ya wanawake ambao walihojiwa na Mwananchi Jumapili walisema huchagua kufanyiwa upasuaji kwa sababu kuzaa kwa njia ya kawaida kunaharibu maumbile katika sehemu zao za siri.

Naye Mwajuma Madolola alisema alijifungua kwa upasuaji kwa kuwa alipata shinikizo la damu saa za mwisho, na hivyo akashindwa kusukuma.

Madaktari wanasemaje?
 Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Muhimbili(MUHAS), Profesa Siriel Massawe, alikiri kuwa kuna ongezeko la upasuaji kwa wajawazito.

“Miaka ya 1990  ni asilimia 12 tu ya wajawazito waliofanyiwa upasuaji, lakini miaka ya hivi karibuni imefikia asilimia 40,” alisema.

   Profesa Massawe alitoa ufafanuzi wa kina kuhusu sababu za upasuaji na kusema, ili mjamzito ajifungue kwa upasuaji ni lazima kuwepo kisababisha cha hatari aidha kwa mama au kwa mtoto.“Inawezekana nyonga ni ndogo na mtoto mkubwa, sababu nyingine ni kifafa cha mimba au ukaaji vibaya  wa mtoto katika mji wa mimba,” alisema
Aliongeza kuwa mwanamke kuvuja damu nyingi kabla ya kujifungua na wakati mwingine shinikizo la damu, au mtoto kuchoka (foetal distress).

“Sababu zipo nyingi, lakini ni lazima sababu ihakikishiwe na kuthibitishwa na daktari ndipo mama afanyiwe upasuaji,” alisema.

Kuhusu wanawake wanaochagua kufanyiwa upasuaji bila sababu za kitabibu, Profesa Massawe alisema wasilaumiwe wajawazito peke yao, bali hata wahudumu wa afya ambao wanatakiwa kulikataza kwa nguvu jambo kama hilo na wanawajibika kuwaelimisha vyema wanawake na jamii kwa ujumla kuhusu athari za upasuaji haswa kukiwa hakuna sababu stahiki.

  “Ni vyema jamii ielewe kuwa wanawake walio wengi  wanaweza kujifungua salama kwa njia ya kawaida,” alisisitiza Profesa Massawe.  Asilimia ndogo tu wanapata matatizo ambayo yanahitaji  wazalishwe kwa upasuaji ili kuokoa maisha ya mama au ya mtoto.   Profesa huyo alisema jambo la muhimu ni kuhakikisha kwamba kila mwanamke anapokuwa mjamzito anapata  huduma ya kitaalam.
 “Mhudumu mwenye taaluma ya ukunga atagundua mapema ni mama yupi ana tatizo linalohitaji azalishwe kwa upasuaji,” alisema Profesa Massawe.

Alisema ni vizuri elimu ya afya ya uzazi itolewe kwa kina ili kuepusha dhana potofu katika jamii na kwamba, ieleweke kuwa kuzaa kwa njia ya kawaida ni salama kwa mama kuliko kuzaa kwa upasuaji.   Kuhusu upasuaji kwa mjamzito ambaye amewahi kujifungua kwa njia hiyo, alisema si lazima afanyiwe upasuaji tena katika kama sababu za awali hazijajirudia.

  Akizungumzia wanawake wanaoishi na Virusi vya Ukimwi, Profesa Massawe alisema wanaweza kujifungua salama na kwa njia ya kawaida iwapo tu watafuatilia tiba.
 “Mama mwenye VVU akijifungua kwa njia ya kawaida atapunguza uwezekano wa  kumwambukiza mtoto kama atahudhuria kliniki yake maalum ya Kuzuia Maambukizo ya Mama kwa Mtoto (PMTCT) na kupewa ushauri nasaha na tiba ya kupunguza makali ya VVU,” alifafanua.

 Aliongeza kuwa, “Huduma  za afya zisipotolewa kwa umakini zitaongeza idadi ya upasuaji usiostahiki. Hii inaathiri ubora wa huduma. 

Aidha alishauri wajawazito kupewa dawa za kupunguza maumivu ya uzazi, kama  sindano ya ‘spinal analgizia’ au tembe.    Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Dk Meshack Shimwale alisema kuongezeka kwa upasuaji kunatokana na masharti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya  kupunguza vifo vya mama na mtoto.
 Dk Meshack, ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya mfumo wa upumuaji, alisema WHO inazitaka nchi zinazoendelea kufikisha angalau asilimia 12 ya upasuaji.

 “Tunafanya upasuaji kwa kuwa, tunatakiwa tuokoe maisha ya mama na mtoto. Huduma za upasuaji zinatolewa bure ili kupunguza vifo hivyo,” alisema Shimwale
Alizitaja sababu zinazosababisha Hospitali ya Amana kufanya upasuaji kwa asilimia kubwa kuwa ni kutaka kufikia malengo ya WHO.

 “Tumepata chumba chenye vifaa vyote cha kufanyia upasuaji kwa hiyo tumeongeza huduma hiyo,” alisema.   Aliongeza kuwa upasuaji huo hufanyika  kama kuna sababu za msingi kama vile ukubwa wa mtoto na nyingine.
Alisema sababu nyingine ambayo imesababisha kuwapo ongezeko la wajawazito kujifungua kwa upasuaji katika hospitali hiyo ya Amana ni hospitali ya rufaa, hivyo wajawazito wanaoshindikana katika hospitali ndogo huletwa hapo.  
Mtindo wa maisha Sababu nyingine kwa mujibu wa Dk Shimwale  kutokana na mfumo wa maisha kama vile wajawazito kutofanya mazoezi kutozingatia masharti.

“Wajawazito hawafanyi mazoezi,  hawafuati masharti na elimu wanayopewa na wakunga. Siku hizi wanakula vizuri tofauti na zamani, kwa hiyo watoto wanakuwa wakubwa,” alisema. 
               Habari na Na Florence Majani wa Mwananchi, Picha na blog editor wetu.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate