Mama mzazi wa miss Tanzania 2006, Wema Sepetu
ametakiwa kufunga mdomo kwa kumwongelea mwanaye hasa kwenye matatizo yake na
mastaa wenzake.
Hayo yamezemwa na watu kwa kutumia mtandao wa bbm
ambapo watumaji walikuwa wakimshauri mwanamke huyo baada ya matamshi yake ya
siku ya jumanne ambapo alimchana msanii mpinzani na mwanaye, Jackline wolper.
Mama na mwana katika picha ya pamoja.
Katika maelezo yake ambayo yalitolewa kwa sehemu
kwenye kipindi cha take one cha zamaradi mketema, mama wema alimgusia wolper
kwa kusema kwamba asimseme mwanaye kuhusu pa kulala kwani anapo na pazuri sana.
Watu walioangalia kipidni hicho walimtaka mama huyo
kuachana na mambo ya watoto kwani mastaa wa bongo ndiyo zao, leo wanakuwa
marafiki, kesho hapakaliki.
Kwa upande wake Wolper alisema hajui nini kinaendelea kati yake na wema kwani yeye anaishi maisha yake na hamfuatifuati mtu, lakini kila kukicha anasakamwa.

“Mimi sijui nini kinaendelea, mbona naishi maisha
yangu mwenyewe, lakini kila kukicha nasemwa vibaya, da!” alisema Wolper.
Nilimsikia Mama Wema alivyonipasha maana ilikuwa bonge la mpasho. Mimi siwezi kujibizana na mama yakeWema, yeye ni kama mama yangu maana ana umri mkubwa kumzidi hata mama yangu mzazi, kujibizana nae ni kujivunjia heshima na kumvunjia heshima yeye pia, hilo sintaweza kabisa dada Irene!
Japo naona ingependeza mama yetu huyu angetuita na kutuweka chini kujua nini tatizo. Mimi nina wazazi na nina ndugu lkn hata siku moja hawawezi kabisa kwenda kwenye vyombo vya habari na kuongelea au kuingilia ugonvi wa mimi namarafiki zangu.
Kuna siku nyingine Irene Uwoya na huyo Wema walikwenda kunitukana kwenye Tv fulani. hiyo pia nilidharau, sipendi kujidhalilisha kwa maneno maneno ya mitaani nisiyojua hasa yanalengo gani! nina shughuli nyingi za kufanya kamwe siwezi kujibizana nao.
alisema Jaque.

No comments:
Post a Comment