Alonso aliifungia Uhispania bao la kwanza dakika ya 20 na la pili la penalti dakika ya 91
Mabingwa watetezi wa Euro 2012
waliweza kuishinda Ufaransa magoli 2-0, timu ambayo wakati mwingine
ilionyesha ustadi wao katika mchezo, lakini kwa jumla wakiwa dhaifu na
kukosa mbinu walipolifikia lango la wapinzani wao.
Uhispania, baada ya ushindi huo katika uwanja wa
Donetsk usiku wa Jumamosi, sasa itakutana na Ureno katika mechi ya nusu
fainali.
Jordi Alba, kwa haraka haraka alifanikiwa
kumchenga mlinzi aliyemuandama na kuupiga mpira juujuu, na ambao
ulimfikia Xabi Alonso, ambaye pasipo kusita alikuwa ameusubiri kwa
makini, na kuusindikiza kwa kichwa hadi wavuni, akiandikisha bao la
Uhispania baada ya dakika ya 20 za mchezo.
Kwa kawaida Xabi Alonso huwa hakosi kufunga
mikwaju ya penalti inapojitokeza, na katika dakika ya 91, aliweza
kufunga bao la pili, na akiuelekeza mpira hadi kona ya lango.
Kwa mbinu hafifu Ufaransa ilijitahidi kuitisha
Uhispania, lakini juhudi zao za pekee zilizokaribia kuandikisha bao ni
wakati Mathieu Debuchy alipousindikiza mpira kwa kichwa kuelekea wavuni
baada ya kupigiwa mpira na Franck Ribery.
No comments:
Post a Comment