EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, June 12, 2012

UKOSEFU WA USINGIZI NI HATARI KWA AFYA YAKO

KITENDO cha kukosa usingizi mara kwa mara wakati wa kulala kuna weza kuonekana ni jambo ambalo halina madhara kiafya, lakini ukweli ni kwamba unapokosa usingizi, hasa kwa muda mrefu, kuna athari kubwa katika afya yako yote, hata kama unakula na kufanya mazoezi vizuri.

Madhara ya ukosefu usingizi huathiri mfumo mzima wa mwili, mathalan, mbali ya kuathiri kinga ya mwili na kuongeza hatari ya kupatwa na magonjwa ya saratani, ukosefu wa usingizi huweza kusababisha madhara mengine yafutayo:

HATARI YA KUPATWA NA UGONJWA WA MOYO
Unapokosa usingizi, mfumo wa uzalishaji homoni huvurugika ambapo uzalishaji wa homoni za

‘stresi’ (stress hormones) huongezeka. Pia husababisha vidonda vya tumbo na hali ya kusikia njaa hata kama umetoka kula muda mfupi. Uko hatarini kusumbumbuliwa na hasira na ghadhabu kila mara.
ONGEZEKO LA SHINIKIZO LA DAMU
Ukosefu wa usingizi huchangia pia ongezeko la shinikizo la damu, pia huchangia kuzeeka kwa mtu kutokana na kuvurugika kwa uzalishaji wa homoni za ongezeko la umri. Humfanya mtu kuonekana mzee ili hali bado ana umri mdogo.
KUZIDISHA TATIZO LA UKOSEFU WA CHOO
Ukosefu wa usingizi huchangia pia tatizo la ukosefu wa choo na huweza hata kusababisha kifo kama tatizo likiwa sugu.

EPUKA KUTUMIA DAWA ZA USINGIZI
Kama unasumbuliwa na tatizo la ukosefu wa usingizi, jua kwamba hauko peke yako. Utafiti uliofanywa hivi karibuni nchini Marekani na Taasisi ya Taifa ya Usingizi (National Sleep Foundation –NSF), umegundua kuwa kati ya watu 10, ni wanne tu hupata usingizi mzuri kila wiki.
Pamoja na kuonekana kwa athari nyingi za kukosekana kwa usingizi, lakini utakuwa unajiweka katika madhara na hatari zaidi iwapo utalazimisha kupata usingizi kwa kumeza dawa za usingizi, kwa sababu ni hatari na mara nyingi dawa hizo huwa hazisaidii kuondoa tatizo.

JINSI YA KUFANYA ILI UPATE USINGIZI
Kwa asili yake, kichocheo cha usingizi mwilini kijulikanacho kama ‘melatonin’ hupatikana kwa ulaji wa mboga za majani na matunda mbalimbali ya kuongeza virutubisho mwilini na hupatikana pia kwa kupata mwanga wa jua wa kutosha wakati wa mchana. Hivyo huna haja ya kumeza vidonge badala yake zingatia uzalishaji wa kirutubisho hicho kwa mlo na mwanga wa jua.
Ili kujiwekea mazingira mazuri ya kupata usingizi mzuri, unashauriwa kuepuka kufanya yafuatayo muda mfupi kabla ya kupanda kitandani kulala:

Epuka kuangalia TV au kompyuta muda mfupi au saa moja kabla ya kulala, kwani teknolojia hizi siyo nzuri sana kwa macho kutokana na mwanga wake, hasa kwa mtu mwenye matatizo ya kupata usingizi.
Epuka kulala huku taa inawaka, hakikisha unalala huku taa zote zikiwa zimezimwa, licha ya mwanga wa taa usiku kusababisha madhara mengine, lakini huchangia kuharibu mtiririko wa usingizi. Hata uamkapo usiku kwenda msalani, ikiwezekana usiwashe taa ili kuepuka kuvuruga usingizi wako.

Usilale karibu na vifaa vya umeme na vyenye sumaku kama vile saa, simu, au redio kwani huchangia kudhoofisha uzalishaji wa homoni za usingizi. Hata saa yako yenye ‘alarm’ ya kukuamsha, unashauriwa kuiweka mbali nawe kabisa.
Mwisho, hakikisha unakuwa na ratiba ya kulala inayoeleweka na hakikisha unalala muda huohuo kila siku. Kwa kawaida mtu anatakiwa kulala kati ya saa tatu na saa nne usiku. Iwapo utazingatia vyote vilivyoelezwa hapo juu, bila shaka utaweza sasa kulala usingizi mnono.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate