EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, July 19, 2012

ATLETICO WAIPELEKA YANGA ROBO FAINALI, AZAM KUNDI LAO SASA NI KUFA NA KUPONA

Wachezaji wa Atletico wakishangilia ushindi wao kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Yanga. Leo wameua 5-0.

ATLETICO FC ya Burundi imeendeleza ubabe kwenye mechi za Kundi C, za Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, baada ya leo kuwafunga mabao 5-0 Waw El Salaam kutoka Sudan.
Waw Salaam waliofungwa na Yanga 7-1, sasa rasmi wameaga mashindano hayo baada ya kupoteza mechi zote tatu, ya kwanza wakifungwa 7-0 na APR ya Rwanda.
 
Kwa matokeo hayo, sasa Atletico inaendelea kuongoza Kundi C, kwa pointi zake saba, baada ya kucheza mechi tatu, kushinda mbili na kutoa sare moja, wakati APR ya Rwanda inashika nafasi ya pili kwa pointi zake nne na Yanga ni ya tatu kwa pointi zake tatu, huku Waw Salaam ambayo haina pointi na imemaliza mechi zake.
Kesho Yanga na APR watahitimisha michezo ya kundi hilo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mechi inayotarajiwa kuwa kali na ya kusisimua.
 
Katika Kundi B, Tusker ya Kenya, imetoka sare ya bila kufungana na Mafunzo ya Zanzibar, hivyo kulifanya kundi hilo, ambalo kuna Azam FC pia lizidi kuwa gumu. Keshokutwa Tusker na Azam FC zitakamilisha mechi za kundi hilo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, katika mchezo ambao timu itakayoshinda moja kwa moja itaungana na Mafunzo kutinga Robo Fainali.
Hatima ya Mafunzo kucheza au kutocheza Robo Fainali inashikiliwa na mechi hiyo, kwani iwapo timu hizo zitatoka sare ya kuanzia mabao 2-2 zitakwenda zote Nane Bora na wawakilishi wa Zanzibar watarejea nyumbani.
 
Mechi za Kundi A, zilichezwa jana na mabingwa wa Tanzania Bara, Simba SC walijiweka kwenye nafasi nzuri ya kwenda Robo Fainali, baada ya kuichapa Ports ya Djibouti mabao 3-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Shujaa wa Simba katika mchezo huo, alikuwa mshambuliaji mpya kutoka Ruvu Shooting ya 
 
Pwani, Abdallah Juma aliyeingia kuchukua nafasi ya Amri Kiemba mwanzoni mwa kipindi cha pili aliyefunga mabao mawili dakika za 60 na 73 na Felix Mumba Sunzu Jr. aliyefunga moja kwa penalti dakika ya 64 
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika bila nyavu za Ports kutikisika, na katika kipindi hicho Sunzu, mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, alipoteza nafasi tatu za wazi mno, za kufunga mabao akiwa amebaki yeye na kipa, Kalid Ali Moursal.
 
Mabadiliko yaliyofanywa na kocha Mserbia, Milovan Cirkovick kipindi cha pili kuwaingiza Juma Nyosso kuchukua nafasi ya Haruna Shamte, Abdallah Juma aliyechukua nafasi ya Kiemba na baadaye Uhuru Suleiman kuchukua nafasi ya Haruna Moshi ‘Boban’ yaliisaidia Simba.
Kwa matokeo hayo, Simba imefikisha pointi tatu baada ya kucheza mechi mbili na sasa inashika nafasi ya tatu kwenye Kundi A, nyuma ya URA yenye pointi sita na AS Vita yenye pointi tatu na wastani mzuri wa mabao. Simba itamaliza na AS Vita ya DRC, mechi ambayo itakuwa kali kwa sababu timu zote zina pointi sawa.  
 
Katika mchezo wa awali uliotangulia wa kundi hilo, URA ya Uganda, ilikuwa timu ya kwanza kufuzu Robo Fainali ya baada ya kuichapa mabao 3-1, AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii.
Mabao ya URA yaliwekwa kimiani na Sula Bagala mawili na Robert Ssentongo, wakati la kufutia machozi la Vita, inayofundishwa na kocha w zamani wa Yanga, Raul Jean Pierre Shungu lilifungwa na Mutombo Kazadi.
MISIMAMO YA MAKUNDI KOMBE LA KAGAME:
KUNDI A:
                     P   W  D   L   GF      GA     GD     Pts
URA             2   2   -     -     5         1         4         6
AS Vita        2   1   -    1     8         3         5         3       
Simba          2   1   -    1     3         2         1         3
Ports            2    -    -    2     -         7         -7        -
KUNDI B:
                     P   W  D  L   GF      GA    GD     Pts
Mafunzi        2   -    2   -    1         1         -         2
Azam FC     1   -    1   -    1         1         -         1       
Tusker FC   1   -    1   -     -         -          -         1
KUNDI C
                     P    W   D   L    GF    GA    GD     Pts
Atletico        3     2    1    -     7       -         7         7
APR             2     1    1    -     7       -         7         4       
Yanga          2     1     -    1    7       3        4         3
Waw            3      -     -     3    -       19      -19      0

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate