Watanzania
waliokuwa wakimbizi katika kambi ya Mogadishu wakielekea kupanda mabasi
maalum yaliyoandaliwa na Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa
Mataifa baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani
Karume jana. (Picha na Juma Mohammed, MAELEZO Zanzibar)
Wazanzibari
waliokuwa wakiishi Somali kama wakimbizi wamerejea nyumbani jana na
kupokelewa na ndugu na jamaa zako katika uwanja wa ndege wa Zanzibar.
Hali ya ulinzi ulikuwa imeimarishwa na maafisa wa usalama ambapo haikuwa
rahisi kwa waandishi wa habari na wapiga picha kuwasogela hadi
walipotoka ndani ya ndege mbili maalumu za Umoja wa Mataifa (UN)
zilizowaleta.
Sura za wa wageni hao na wapokeaji zilisajika baada ya kufika uwanja huo ambapo baadhi ya watoto wakionekana wakilia muda mfupi baada ya kutua huku wazazi wao wakiwa na furaha na kukanyanga tena nyumbani.
Wakizungumza na waandishi wa habari walionesha hisia zao za kufuwahia kurudi nyumbani na kusikitika kuwa baadhi ya wenzao wamekataa kurudi kutoka na kupata taarifa za maandamano yaliotokea Mei 27 mwaka huu na kusababisha mali kuharibiwa na baadhi ya watu kushitakiwa.
“kwa kweli watu wengi walikuwa tayari kujisajili na UNHCR tayari kurudi nyumbani lakini kitu kilichowarejesha nyuma wenzetu ni baada ya kusikia maandamano na baadhi ya matukio ya hivi karibuni kuzuwiwa kwa mihadhara na baadhi ya watu kushitakiwa….kwa hivyo wakaogopa akiamini hali haijatulia bado” alisema Mohammed Suleman na kuongeza.
“Nimefurahi sana kurudi nyumbani lakini changamoto pekee ni kuanza maisha mapya japo tumepewa msaaada na shirika la UN” alisema Mohammed Suleiman.
Soma zaidi: zanzibaryetu.wordpress.com

Watoto
ambao kwa sasa ni Raia wa Somalia wakiwa na wazazi wao Raia wa Tanzania
waliokuwa wakimbizi nchini Somalia wakisubiri taratibu za Uhamiaji
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume jana baada ya
kuwasili wakitokea Mogadishu na ndege ya Umoja wa Mataifa chini
uangalizi wa UNHCR. (Picha na Juma Mohammed, MAELEZO Zanzibar)
Baadhi
ya Wanzania 38 waliokuwa wakimbizi Jijini Mogadishu wakielekea sehemu
ya mapokezi mara baada ya kushuka katika ndege la Umoja wa Mataifa
iliyowaleta nyumbani wakiwa na wake zao walioa nchini Somalia baada ya
kuishi huko kwa miaka 11,walikimbia vurugu za Januari 26/27 mwaka 2001
(Picha na Juma Mohammed, MAELEZO Zanzibar)
No comments:
Post a Comment