Nje ya
mahakama inayisikiliza kesi ya mtoto wao, mama Lulu na baba Lulu walijikuta
wakiingizwa kwenye midomo ya watu waliofurika mahakamani hapo wakiwashauri
waondoe tofauti zilizopita na kurudiana ili kumfanya mtoto wao, Lulu ambaye
anahusishwa na kifo cha mcheza filamu Steven Kanumba kilichotokea mwezi aprili
mwaka huu.
Elizabeth Michael 'Lulu'akiwa na Mama yake
Baadhi
ya watu walisema katika kipindi hiki kigumu wazazi hao wa Lulu wangerudiana
katika mshikamano wa maisha kitendo ambacho kingemfariji sana binti yao na
kujipa moyo katika kipindi hiki cha kesi yake kusikilizwa.
“Sasa
baba anaishi kivyake Arusha sijui Moshi, mama anakaa Tabata Dar si wangerudiana
tu. Haya mambo yaliyompata mtoto wao yanataka ukaribu wa wazazi endapo wote
wapo hai,” alisema mzee mmoja akipokuwa akizungumza na mwenzake kuhusu wazazi
hao.
Wengine
walimsifu mzee Michael kwa kitendo chake cha kuhudhuria siku ya kesi jijini Dar
es Salaam kwani kwa mazazi mwingine angeweza kupotezea kutokana na umbali pia
uchumi wan chi ambao si mzuri sana kwa miaka ya hivi karibuni.
BABA mzazi wa msanii wa filamu, Elizabeth Michael 'Lulu'
Lakini
wapo waliodai mahakamani hapo kwamba wazazi hao hawakuwahi kuishi pamoja kama
mke na mume bali walikuwa wapenzi na baadaye mama Lulu akajikuta amebeba
ujauzito wa mwanaume huyo.
No comments:
Post a Comment