Lulu akiwapungia mkono bibi yake, ndugu na jamaa.
Na Richard Bukos
HUKU kesi ya kushukiwa kuhusika na mauaji ya marehemu Steven Kanumba ikiendelea kumkabili nyota wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, bibi yake na msanii huyo alitinga kortini kusikiliza kesi ya mjukuu wake.

Bibi
huyo ambaye alitajwa kwa jina moja la Elizabeth, ilielezwa ni mama mzazi
wa mama wa msanii huyo Lucresia Karugila, alitinga katika Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam, juzi, Jumatatu, jijini Dar es Salaam akiwa
ameongozana na mwanaye (mama’ke Lulu) na ndugu wengine.
Shauri hilo lilifikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza uamuzi wa kupelekwa Mahakama ya Rufaa, kama mawakili upande wa serikali walivyoomba katika kesi hiyo.

“Huyu ni bibi yake Lulu, amekuja kutokea kijijini Bukoba.
Ni mama yangu mzazi. Ameguswa na jambo hili na ameona ni vyema aje
kumuona mjukuu wake,” alisema mama Lulu.
Kesi hiyo imehairishwa na Msajili wa Mahakama hiyo, Amiri Msumi, mpaka Agosti 20 mwaka huu kwa vile jaji aliyetakiwa kusikiliza kesi hiyo Twalib Fauz hakufika mahakamani hapo kwa kile kilichoelezwa alikuwa na dharura. Lulu alirudishwa mahabusu katika Gereza la Segerea kusubiri tarehe hiyo.

No comments:
Post a Comment