MBOWE ASEMA MPANGO HUO UNARATIBIWA NA KIGOGO WA USALAMA WA TAIFA, MKUCHIKA ASEMA NI TUHUMA NZITO, AZIVUTIA KASI
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),kimetoa tuhuma nzito kikidai kigogo mmoja (jina tunalo) wa Idara ya Usalama wa Taifa anaratibu mpango wa kuwaua viongozi wake waandamizi akiwamo Katibu Mkuu, Dk Willbrod Slaa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),kimetoa tuhuma nzito kikidai kigogo mmoja (jina tunalo) wa Idara ya Usalama wa Taifa anaratibu mpango wa kuwaua viongozi wake waandamizi akiwamo Katibu Mkuu, Dk Willbrod Slaa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika.
Kwa sababu hiyo, chama hicho
kimeitisha kikao cha Kamati Kuu (CC) leo kujadili mambo mbalimbali na
Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe amesema ajenda kuu itakuwa kuzungumzia
usalama wa viongozi wao kutokana na vitisho hivyo.
Kuhusu tuhuma hizo, Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika amesema tuhuma hizo ni
nzito na atazijibu kwa maandishi.
Katika mkutano wake na waandishi wa
habari uliofanyika Dar es Salaam jana, Mbowe alitaja majina ya baadhi ya
maafisa idara hiyo (majina tunayahifadhi) na kudai kuwa mmoja kati yao
ndiye anayeratibu shughuli hiyo na tayari yupo mjini Dodoma kwa ajili ya
kuongoza kundi linalotaka kumdhuru Mnyika.
Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi
ya Upinzani Bungeni, alisema mbali na viongozi hao wawili, mwingine
aliyedai kuwa anafuatiliwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu, Godbless Lema akidai
kwamba, taarifa zinaonyesha kuwa wanafuatiliwa kwa saa 24.
Mbowe alidai kwamba idara hiyo ambayo
haifanyi shughuli za siasa, inatumia ofisi yake vibaya kwa kufuatilia
viongozi hao wakidhani chama hicho kina mambo ya siri kinayotaka
kuyafanya katika nchi hii.
“Sisi Chadema hatuna mambo ya siri
tunayotaka kufanya katika nchi hii. Matatizo ya Watanzania yapo wazi na
yanajulikana na kila mmoja, Serikali ya CCM itekeleze sera na ahadi zao
kwa wananchi na si vitisho,” alisema Mbowe na kuongeza:
“Tunaomba wananchi waelewe kuwa
viongozi wao wako hatarini, lakini Chadema hatutarudi nyuma katika
kutetea haki za wanyonge hata kwa kufa na hatuwezi kupeleka malalamiko
yetu polisi sababu nao ni sehemu ya tatizo.”
Alisema chama chake kimekuwa
kikihusishwa na mambo mengi ukiwamo mgomo wa madaktari unaoendelea na
kusema Chadema hakiko nyuma ya mgomo huo na hakijawahi kukutana na
kufanya kikao na madaktari.
“Wametuhusisha na mambo mengi na sasa
wanasema tuko nyuma ya mgomo wa madaktari, taarifa hizo siyo za kweli
na wala hatujawahi kukaa nao kikao chochote kujadili masuala yao,
madaktari wana madai ya haki zao. Hapa tunaingia kwenye utaratibu wa
kutesana ili kupata taarifa, mmesikia Dk Ulimboka aliteswa ili aseme
Chadema iko nyuma ya mgomo,” alidai Mbowe.
Hata hivyo, Mbowe alisema suala la
kutokuwa nyuma ya mgomo huo haliwanyimi fursa ya kutetea makundi ya watu
wanaodai haki zao wakimwamo madaktari na kusema anaunga mkono tamko la
viongozi wa dini.
“Viongozi wa dini wametoa tamko lao
jana (juzi), wakitaka Serikali kuwarudisha madaktari na kumalizia suala
hilo kwa njia ya mazungumzo,” alisema.
Alisema Chadema kinaunga mkono tamko hilo akisema si busara kuwa fukuza kwa sababu Serikali imetumia gharama kuwaandaa.
Dk Slaa anena
Kwa upande wake, Dk
Slaa alisema Chadema kimeamua kutotoa madai yake polisi akidai kuwa
imepokea madai mengi kutoka kwa viongozi na wanachama ya kutendewa
visivyo lakini hakuna hata moja lililowahi kufanyiwa kazi.
Kuhusu kitisho la kuuawa alidai kwamba alianza kutishiwa siku nyingi na kusisitiza kuwa hilo haliwezi kuwanyamazisha.
Kuhusu kitisho la kuuawa alidai kwamba alianza kutishiwa siku nyingi na kusisitiza kuwa hilo haliwezi kuwanyamazisha.
“Taarifa za sasa wanaanza na Mnyika
na kufuatia mimi, ninachosema wafanye watakavyo hatutaacha kufanya kazi
yetu, hata nilipoibua tuhuma za EPA niliwaambia watuhumiwa wengine wa
sakata hilo ni Usalama wa Taifa,” alisema Dk Slaa.
Dk Slaa alitaja baadhi ya mambo
ambayo alidai kuwa hayakushughulikiwa yalipowasilishwa polisi kuwa ni
vinasa sauti alivyowekewa kwenye chumba alichokuwa amelala wakati wa
vikao vya Bunge Mjini Dodoma.
Alisema vifaa hivyo vilichukuliwa na
polisi kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi lakini hadi leo hakuna taarifa
iliyotolewa hata kwake licha ya kuwa mhusika mkuu.
Mnyika: Namwachia Mungu
Akizungumzia
madai hayo, Mnyika alisema anamuachia Mungu kwa kuwa ndiye aliyetoa
uhai hata kwa hao wanaofikiria kutekeleza kitendo hicho.
Mnyika alidai kuwa baada ya kupata
taarifa hizo ambazo alisema zimeandaliwa kwa ama kunyeshwa sumu au
kuvamiwa na majambazi, alikutana na familia yake na uongozi wa chama
chake ambao kwa pamoja wamemtaka aendelee na kazi ya kutetea rasilimali
za taifa.
“Nilipopata taarifa hizi nimekutana
na viongozi wangu wa chama na jana usiku (juzi), nilikutana na familia
yangu, kwa pamoja wameniambia niendelee na kazi hii ninayoifanya kwani
nimetumwa na wananchi na sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, ”alisema
Mnyika.
Kwa upande wake, Lema alisema
taarifa za kufuatiliwa na watu hao wanaodaiwa kuwa ni wa Usalama wa
Taifa alizipata kwa mmoja wa vyanzo vyake kutoka serikalini.
“Nilipigiwa simu na mtu mmoja kutoka
serikalini aliyeniambia kuna gari nyuma linanifuatilia, nilipogeuka
niliona na kusimama kisha nikashuka na kubadili gari na lenyewe
likaendelea kunifuatilia katika gari nililokuwa nimepanda,” alidai
Lema.
Lema alidai kwamba hata juzi asubuhi alikutana nalo katika nyumba aliyofikia na alipolikaribia watu hao walishusha vioo na kumsalimu wakimwita ni Mbunge wa Arusha aliyeko kwenye likizo.
Lema alidai kwamba hata juzi asubuhi alikutana nalo katika nyumba aliyofikia na alipolikaribia watu hao walishusha vioo na kumsalimu wakimwita ni Mbunge wa Arusha aliyeko kwenye likizo.
SOURCE MWANANCHI
No comments:
Post a Comment