Mratibu
Mkazi wa Umoja Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou (katikati) akiwasili
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere kumpokea
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Asha Rose Migiro aliyemaliza
muda wake siku ya jana wakati akirejea nchini Tanzania. Kushoto ni Afisa wa
Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini Hoyce Temu.
Baadhi
ya Mabalozi, Wahadhiri na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
pamoja na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa wakiwa wamejipanga kumpokea Dkt. Asha Rose Migiro.
Msafara
wa Dkt. Asha Rose Migiro ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje
Mh. Benard Membe (gari la pili) kuelekea sehemu maalum ya mapokezi.
Dkt. Asha Rose Migiro akishuka kwenye gari yake baada ya kukanyaga Ardhi ya Tanzania.
Dkt.
Asha-Rose Migiro akipokelewa kwa shangwe na zawadi za maua kutoka kwa
ndugu, jamaa, marafiki na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje
waliofika kumlaki.
Dkt.
Asha Rose Migiro akisalimiana na baadhi ya mabalozi wapya walioteuliwa
na Mh. Rais hivi karibuni. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa
nchini Dkt. Alberic Kacou.
Dkt.
Asha Rose Migiro akiendelea kusalimiana na Baadhi ya Mabalozi. Kushoto
ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe
sambamba na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou.
Waziri Membe na Dkt. Migiro wakielekea kwenye chumba maalum cha mapumziko kabla ya mkutano na waandishi wa habari.
Dkt.
Asha Rose Migiro (katikati), akizungumza na waandishi wa habari nchini
Tanzania baada ya kumaliza muda wake kama Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa ambapo pamoja na mambo Mengi amesisitiza kwamba hatojihusisha na
siasa kwa sasa. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa Mh. Benard Membe na Kulia ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa
nchini Dkt. Alberic Kacou.
Dkt.
Asha Rose Migiro akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa
habari baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius
Nyerere. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mh. Bernard Membe.
Dkt.
Asha Rose Migiro (katikati) akiteta jambo Waziri Membe sambamba na
Viongozi mbalimbali wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakiongozwa
na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberi Kacou (kushoto)
waliofika kumlaki katika Uwanja wa Ndege wa Mwl. J.K Nyerere.
Mbunge
wa Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji akimpongeza Dkt. Asha Rose Migiro
kwa kazi nzuri alipokuwa akitumikia kama Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa walipokutana siku ya jana katika Uwanja wa ndege.
Pichani
Juu na Chini ni wakinamama wakimwimbia Happy Birthday Dkt. Asha Rose
Migiro ikiwa ni maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa aliporejea nyumbani siku ya jana.
Kikundi cha Ngoma kikitoa burudani kwa Dkt. Migiro (hayupo pichani)
Dkt.
Asha Rose Migiro akizungumza Jambo na Dkt. Alberic Kacou wakati
wakitizama burudani ya ngoma iliyoandaliwa maalum kwa ajili yake.
Kushoto ni Waziri Membe.
Dkt. Migiro akiwasalimia wasanii wa kikundi cha ngoma.
"Karibu tena Nyumba Mama"... Waziri Membe akiagana na Dkt. Asha Rose Migiro baada ya mapokezi.
Dkt. Asha Rose Migiro akiagana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dkt. Alberic Kacou.
Dkt.
Asha Rose Migiro akiondoka katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl.
Julius Nyerere sambamba na ulinzi mkali wakiwemo maafisa wa kimataifa
kutoka Ufilipino waliohakikisha ametua nchini Salama.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) ambaye amemaliza muda wake, Dkt. Asha Rose Migiro, amerejea nyumbani siku ya jana na kusema kwamba anatarajia kurudi kufundisha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alikuwa akifundisha kabla ya kuingia kwenye ulingo wa siasa.
Kinyume na matarijio ya watu wengi, Dkt. Migiro amesema kuwa kwa sasa hatarajii kujishughulisha katika mambo ya siasa na wala hana mipango ya kugombea urais siku za mbele.
Amesema kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amamteua kuwa Balozi Maalum wa Malaria katika Bara la Afrika na kuongeza kuwa pamoja na kwamba shughuli hizo atakuwa anazifanya kwa muda wake mchache, bado kuna uwezekano mkubwa zikambana na kushindwa kujishughilisha na mambo ya kisiasa.
No comments:
Post a Comment