Marehemu Kati Kerenge enzi za uhai wake.
Baadhi ya waombolezaji wakibeba
jeneza lililowekwa mwili wa merehemu Kati Kerenge kabla ya mazishi yake
yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Jumamosi
Julai 7 jijini humo. Marehemu Kati aliyekuwa Mkuu wa Masoko na
Mawasiliano wa Benki ya Barclays alifariki Julai 1 jijini humo.
Mama mzazi wa marehemu Kati Kerenge,
Professor Apollonia Kerenge (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya
waombolezaji katika misa ya mazishi iliyofanyika katika kanisa la
Prebeterian la Mt. Columbus jijini Dar es Salaam Jumamosi Julai 7 jijini
Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina akizungumza wakati wa misa.
Aliyekuwa Mkuu wa Rasilimali Watu wa
Tanga Cement ambaye marehemu alishawahi kufanya kazi, Bi. Jayne Nyimbo
akizungumza. Kwa sasa Bi Jayne ni Mkuu wa Rasilimali watu wa kampuni ya Twiga Cement.
Mama mzazi wa marehemu Kati Kerenge, Professor Apollonia Kerenge akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu mwanawe.
Mama mzazi wa marehemu Kati Kerenge,
Professor Apollonia Kerenge akiweka maua juu ya kaburi alilozikwa
marehemu Kati Kerenge. Kulia ni mmoja wa marafiki wa karibu wa Kati,
Mwinda Kiula ambaye ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC
Tanzania.
No comments:
Post a Comment