Wema Isaac Sepetu.
Na Shakoor Jongo
WEMA Isaac Sepetu amelidokeza gazeti alipendalo la Ijumaa Wikienda
kuwa ameitwa ikulu ya Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza kwa mwaliko
maalum.
Wema alisema mwaliko huo aliupata mara tu baada ya kuzindua ile filamu yake ya Super Star wiki mbili zilizopita ambapo katika mwaliko huo wa ujumbe kutoka ikulu hiyo ulimuomba kutoisambaza kwanza kabla ya kwenda kuizindua nchini humo.

“Waliniambia juu ya mimi
kuomba uraia wa nchi hiyo ili kukuza filamu zao. Kusema kweli nilikuwa
nina ratiba ya kwenda kuizindua filamu yangu Rwanda, Burundi na Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo. Yaani sijui hata walijuaje. Sijui ni nini
kimetokea, nina wasiwasi. Hata sijui nitaongea nini na Rais wa Burundi,”
alisema Wema na kuongeza kuwa maandalizi yakikamilika atatii wito huo
muda wowote.
No comments:
Post a Comment