Wakati wakithibitisha kuondoka kwa mwamba huyo,
Barca walimishukuru Seydou Keita kwa juhudi zake za kuletea klabu hicho
cha Uhispania mafanikio na vile vile wakamtakia kila lakheri
anakokwenda.
Kwa wakati huu kuna fununu kwamba mchezaji huyo wa Mali huenda anahamia klabu kimoja cha Uchina, Dalian Aerbin
Ikiwa hatiamae ataishia China basi Keita hatakuwa mchezaji wa kwanza kutoka bara la Afrika kufanya hivyo.
Majuzi nahodha wa timu ya Ivory Coast Didier
Drogba aliwafuata Frederic Kanoute na Yakubu Aiyegbeni wa Nigeria
kujiunga na timu za ligi kuu ya China.
Keita, mwenye umri wa 32, alijiunga na Barcelona
mwaka 2008 kutoka Sevilla akiwa ni mchezaji wakwanza kabisa ambaye Pep
Guardiola alimsajili mara tu alipochukuwa uongozi wa Barca.
Kabla ya hapo mchezaji huyo alikuwa Olympic
Marseille, Lorient na Lens zote za Ufaransa na ndio baadaye akahima
Seville ya Uhispania.
Keita amehama baada ya Guardiola luondoka kama
Meneja wa Barcelona na mahali pake kuchukuliwa na aliyekuwa naibu wake
Tito Vilanova
No comments:
Post a Comment