Ule mpambano
uliokuwa na mvuto mkubwa kati ya mastaa wetu wa Bongo, Wema Spetu na Jackline Wolper
uliisha kwa mashamsham na vicheko baada ya kumalizika. Wengi walisema mpaka
mwisho wa kupigana hakuna aliyeibuka mshindi
Lakini kwa
mtu aliyekuwa Uwanja wa Taifa siku hiyo ya Jumamosi ya Julai 7 mwaka 2012 na
kuangalia mazingira ya ndondi kwa umakini anaweza kusema ukweli kwamba Wema
alionyesha dalili za kuogopa kupigwa.
Tangu
pambano hilo lililowatuliza watu katika ukimya mkubwa lianze Wema alionekana
kujikinga zaidi na sehemu za usoni ambapo mashabiki walisema anahofia kudundwa
eneo hilo kwa sababu ya kutumia krimu kuongeza weupe hivyo angepigwa eneo la
uso angewekwa alama ya muda mrefu.
Kila mara
Wema aliweka ngumi usoni wakati Jack alipokuwa akimsogelea na mwisho Wema
alikimbia mbali na kusababisha mashabiki wacheke. Wengine walisema kama
mabondia hao wangepigana kiukweli Wema angepigwa na ni mwoga wa kupigwa ndiyo
sababu jukwaani alikosa ujasiri kuliko mwenzake.
No comments:
Post a Comment