Warembo
wa Redds Miss Sinza wakiwa mazoezini kwenye ukumbi wa Mawela social
(Ten Star Lounge) uliopo karibu na hotel ya Vatican chini ya mwalimu wa,
Mwajabu Juma ambaye anashikiria taji la Top Model . Warembo hao
watapanda jukwaani Julai 13 kutafuta tiketi ya kuiwakilisha Sinza katika
mashindano ya Kanda ya Kinondoni na baadaye Miss Tanzania.
******
Twanga Pepeta kuwachezesha Kisigino Miss Sinza 2012
· Kamati ya Miss Tanzania kutembelea kambi leo
WAKATI
bendi ya African Stars (Twanga Pepeta) itapamba shindano la kumsaka
mrembo wa Redds Miss Sinza 2012 lillopangwa kufanyika Ijumaa kwenye
ukumbi wa Mawela Social (Ten Star Lounge) uliopo karibu na hotel ya
Vatican City, Kamati ya Miss Tanzania leo itatembelea warembo hao kwa
lengo la ‘kuwafunda’ tayari kupanda jukwaani.
Mratibu
wa kampuni ya Calapy Entertainment, Majuto Omary alisema jana kuwa
Twanga Pepeta imeandaa zawadi kwa mashabiki wake na wale wa urembo kwa
kuwapa uhondo wa nyimbo mbili mpya ambazo zitakuwa zinasikika kwa mara
ya kwanza jukwaani.
Nyimbo
hizo ni Mapambano ya Maslahi uliotungwa na Muumin Mwinjuma, Shamba la
Twanga ambao umetungwa na Greyson Semsekwa na mmoja ambao haujapewa
jina uliotungwa na Jumanne Saidi ambaye amfunga ndoa na mnenguaji wa
bendi hiyo, Asha Sharapova. Alisema kuwa nyimbo hizo ni zawadi kwa
mashabiki wa Twanga wa Sinza na vitongoji vyake kwani bendi hiyo
haijafanya shoo huko muda mrefu. “Tunatarajia kuwa na shoo
nzuri kutoka kwa warembo na bendi ya Twanga Pepeta ambayo mwaka huu
imeshinda tuzo mbili katika tuzo za muziki Tanzania,” alisema.
Kuhusiana
na ziara ya Kampuni ya Lino International Agency, Majuto alisema kuwa
Lundenga na wenzake watafanya mazungumzo na warembo hao baada ya
mazoezi yao ya pamoja. Alisema kuwa ziara hiyo ni moja ya faraja kwa
warembo na kamati ya Miss Sinza kutokana na ukweli kuwa ujio wao ni wa
Baraka na hitimisho la mashindano ya vitongoji nchini.
“Miss
Sinza ndiyo inafunga pazia la mashindano ya Vitongoji (vituo) nchini,
Lundenga na wenzake wanakuja kutoa baraka zao kabla ya kuanza
pilikapilika za Redds Miss Tanzania,” alisema. Shindano hilo
lililodhaminiwa na Redds Premium Cold, Dodoma Wine, Kidoti Fashion,
Clouds Entertainment, sufianimafoto.blogspot.com, Lady Pepeta na flexi
P, Fredito Entertainment, Screen Masters, Brake Point na Jackz
Cosmetics Kinondoni.
No comments:
Post a Comment