EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, August 20, 2012

Askofu adaiwa kudanganya uraia wake


                                      Mkurugenzi Mkuu wa Nida, Dickison Maimu
Wenyeji wa Mkoa wa Mbeya wanaoishi jijini Dar es Salaam wamewasilisha barua na vielelezo katika ofisi ya Mamlaka ya Taifa ya Utambuzi (Nida) kupinga Askofu Mkuu wa Kanisa la House of Prayer  Shield of Faith Christian Fellowship, Mulilege Mkombo, anayedaiwa kujiandikisha kama mzaliwa wa Tanzania kwa lengo la kupata kitambulisho cha Taifa.

Katika barua hiyo ambayo imepelekwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Nida, Dickison Maimu, na nakala kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, Edward Lowassa, wameeleza kuwa Askofu Mkombo jina lake halisi ni Mukombo Muyodi aliyezaliwa Aprili 4, mwaka 1964 eneo la Butumba Kimakondolo Lumbumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Imeeleza kuwa askofu huyo katika mchakato wa kupata kitambulisho cha uraia kwa jina la Mulilege Mkombo, amejiandikisha katika Kata ya Boko Magengeni jijini Dar es Salaam kama raia wa Tanzania.

Maimu akizungumza na NIPASHE mwishoni mwa wiki alithibitisha kupokea barua na vielelezo kutoka kwa wananchi hao vya pingamizi dhidi ya askofu huyo na kwamba mamlaka yake kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji vimeanza uchunguzi wa suala hilo.

Kwa mujibu wa barua hiyo iliyoandikwa na kusainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi inayoshughulikia uhifadhi wa mazingira na Idara ya Haki za Binadamu (MRECA), William Mwamalanga, ambayo NIPASHE imefanikiwa kuona nakala yake, imeeleza kuwa askofu huyo siyo mzaliwa wa Tanzania bali amezaiwa DRC.

“Timu yetu ya watafiti imefanya kazi na kubaini pasipo shaka kuwa mtajwa hapo juu ni raia wa DRC hasa baada ya kumuhoji mkewe aitwaye Mary Mukombo ambaye walifunga ndoa yao huko huko DRC na wazazi wao walihusika kufunga ndoa hiyo na kutambuliwa na mamlaka ya DRC,” inaeleza  barua hiyo.

Barua hiyo imezidi kueleza kuwa watafiti wa MRECA wamebaini vyeti vya taaluma na viapo vya kisheria kutoka mamlaka ya DRC na kwamba Askofu Mukombo Muyodi alifanikiwa kughushi vyeti vya kuzaliwa baada ya kununua wazazi mkoani Mbeya na kujiita Mulilege Mukombo Kameka jina ambalo ni maarufu kwa kabila la Wanyakyusa mkoani humo.

“Ikumbukwe ni vigumu kujua nia ya Mukombo Muyodi kununua wazazi na kujipachika jina la Mulilege Mkombo na kumfukuza mkewe huku akitajwa kuwa alikuwa askari wa zamani wa DRC,” imeeleza sehemu ya barua hiyo.

Aidha, taasisi hiyo ya MRECA imewasilisha Nida vyeti vya kuzaliwa vya askofu huyo akiwa DRC, vyeti vinavyodaiwa vya kughushi na pasipoti ya kusafiria hapa nchini.

Mara kadhaa NIPASHE ilimtafuta askofu huyo bila mafanikio, lakini mkewe, Greener Pulin, alizungumza kwa niaba ya mumewe akizungumza na kusema kuwa watu wanaohoji uraia wa askofu baadhi ni waumini wa kanisa hilo ambao wanatumiwa na baadhi ya watu kwa lengo la kumdhoofisa katika utendaji wake wa kazi.

via  Nipashe

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate