Rehema Chalamila ‘Ray C’.
MSANII ‘first class’ wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Rehema
Chalamila ‘Ray C’, amerejea Bongo na kutangaza kusaka mume huku akiweka
wazi vigezo anavyotaka awe navyo, Jelard Lucas anashuka nayo.
Akichonga
na Over The Weekend juzikati, Ray C aliyekuwa amejichimbia nchini
Kenya, alisema mwanaume atakayeweza kupata penzi lake anatakiwa kuwa na
elimu ya kawaida, maendeleo, asiwe mwanamuziki wala pedeshee, awe na
mvuto na mwenye kuyajua vizuri malavidavi.
Mwanadada huyo ‘chakaramu’ aliongeza kuwa mwenye sifa hizo akipatikana, atamzalia watoto wawili na kujenga naye familia bora kwani amechoshwa na maisha ya usela.
Mwanadada huyo ‘chakaramu’ aliongeza kuwa mwenye sifa hizo akipatikana, atamzalia watoto wawili na kujenga naye familia bora kwani amechoshwa na maisha ya usela.
“Sina
mume wala mpenzi, kwa sasa nipo single, ukiniulizia ishu za zamani
ntakushangaa kweli, vigezo ndiyo hivyo, kama kuna mtu yupo tayari
ajitokeze tufunge ndoa,” alisema Ray C.
Kuhusu kurudi kwenye gemu, Ray C aliwaahidi mashabiki zake kuwa baada ya mfungo kumalizika, yupo kwenye harakati za kuzindua albamu yake mpya aliyoipa jina la ‘Moyo Waniuma’ yenye nyimbo 10.
Aliongeza kuwa soko la muziki Bongo ni bovu sana ukilinganisha na Kenya hivyo bado mishemishe zake nyingi atakuwa akizifanyia nchini humo

No comments:
Post a Comment