Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (katikati) akizungumza wakati
alipozindua jarida la ‘SAUTI YA ILALA’ ambapo amesema kwa sasa
halmashauri hiyo inajiendesha kisasa sana, wanakusudia kuwa na jarida
ambalo kweli litafanya kazi ya kuitangaza Ilala, na kufikisha ujumbe si
tu kwa wananchi wa Ilala bali kwa Jamii nzima.
Aidha
amewataka wafanyabiashara wa Ilala kujitangaza katika gazeti hilo ili
fedha zitakazopatikana sio tu zitalipia gharama za uchapishaji bali
fedha zitakazobakia zitatumika kuboresha utoaji wa huduma kwa jamii.
Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Paul Wanga na Kushoto ni
Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala Tabu Shaibu, Mkurugenzi wa Kampuni
361 Mustafa Hassanali, Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Kheri Kessy.
Wageni waalikwa wakipitia toleo la zamani la Jarida la Sauti ya Ilala kabla ya uzinduzi rasmi.
Pichani
Juu na Chini ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (wa
tatu kulia) na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Kheri Kessy wakifungua
pazia kuashiria uzinduzi rasmi wa ‘Jarida la Sauti ya Ilala’.
Wanaoshuhudia tukio hilo Kulia ni Mh.Sada Madwangwa, Kaimu Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ilala Paul Wango na kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya
361 Mustafa Hassanali ambao ndio waandaaji wa uzinduzi huo.
Sasa limezinduliwa rasmi.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (katikati), Naibu Meya wa
Manispaa ya Ilala Kheri Kessy (wa pili kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa
Manispaa wakikata keki yenye mfano wa jarida hilo kwa pamoja mwendelezo
wa uzinduzi wa Jarida hilo.
Wageni waalikwa wakisoma jarida hilo.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakipitia jarida hilo.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (kulia) akipata picha ya
ukumbusho na Mmoja wa wadhamini wa jarida la Sauti ya Ilala Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya GF Trucks & Equipment Ltd. Bw. Imran Karmali
(katikati).
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akimshukuru mmoja wa wadhamini
wa Jarida hilo Meneja Masoko na Afisa Uhusiano wa Benki ya Exim Linda
Chiza.
Manispaa
ya Ilala kwa kuelewa umuhimu wa habari na haki ya wananchi wake
kupashwa habari na kujua mustakabali mzima Manispaa yao imerejesha na
kuzindua upya jarida lake linaloitwa ‘SAUTI YA ILALA’.
Jarida
hilo limebuniwa upya na kuongezwa vionjo vipya vya fani na maudhui
vitakavyo mvutia msomaji ikiwemo habari za manispaa, habari za biashara
ndani ya manispaa nakadhalika.
Akizindua
jarida la ‘SAUTI YA ILALA’ katika ukumbi wa Anatoglo leo jijini Dar es
Salaam, Meya wa Manispaa ya Ilala Mstahiki Jerry Silaa amesema dhima
yake ni kuhakikisha kuwa Ilala inakuwa kitovu cha uchumi wan chi na
kufanya maeneo ya katikati ya mji kuwa sehemu safi, nzuri na inayovutia.
Ameongeza
kuwa kwa kupitia jarida hilo watu wataweza kuona shughuli mbali mbali
za kiuchumi zinazofanyika na pia kuona mafanikio yake.
Naye
Afisa Uhusiano wa manispaa ya Ilala Bi. Tabu shibu akizungumzia Jarida
hilo amesema ‘SAUTI YA ILALA’ mpya inakwenda kugusa wengi kwa sababu
jarida limebuniwa upya kuweza kukidhi matakwa ya watu wa rika, uchumi,
elimu na Nyanja mbambali hivyo wananchi watakaopata fursa ya kulisoma
watafurahia ladha tofauti.
No comments:
Post a Comment