EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, August 13, 2012

MWANAFUNZI AUWAWA KISHA KUFUKIWA KTK SHIMO NYUMA YA CHOO


Mwanafunzi wa Darasa la Saba shule ya msingi Hogolo, aliyefahamika kwa jina la Matha Mazoea Mwenye umri wa Miaka (14)  ameuawa kwa kunyongwa na kufukiwa kwenye shimo nyuma ya nyumba yao karibu na choo baada ya kubakwa.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Zelothe Sephen alisema tukio hilo limetokea mnamo tarehe 11/08/2012 majira ya saa 08:00 asubuhi katika mtaa wa Ikulu Kijiji cha Hogolo Kata ya Hogolo tarafa ya Zoisa Wilaya ya Kongwa.

 “Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi kwani marehemu alikuwa amevunja uhusiano na mpenzi wake wa muda mrefu aliyejulikana kwa jina la Heri Aboubakar na kuanzisha uhusiano na mpenzi wake mpya aliyefahamika kwa jina la Wilfredy Muhaha @ Kabo mwenye miaka (17) “ Alielezea Kamanda Zelothe

Katika tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji hayo ambao ni Asha Jafari Mohamed mwenye umri wa miaka 16, mkulima, mkazi wa Mtaa wa Nyerere Hogolo ambaye ni rafiki wa marehemu na Rino Mazoea mwenye umri wa miaka 21, Mkulima, Mkazi wa Ikulu Hogolo Wilayani Kongwa ambaye ni kaka wa marehemu.
Bw. Zelothe alieleza kwamba  ili kufanikisha uchunguzi wa awali Jeshi la Polisi pia Wilayani humo linamshikilia  mpenzi mpya wa marehemu Bw. Wilfredy s/o Muhaha  pamoja na kumtafuta mpenzi wa zamani wa  marehemu  Bw. Heri s/o Aboubakar ambaye amekimbia kijijini hapo na hajulikani alipo mpaka sasa.

Aidha kamanda Zelothe alisema Katika tukio hilo Kaka wa marehemu ambaye  anashikiliwa na Jeshi la Polisi, katika maelezo yake ya awali alidai kusikia  purukushani zikitokea usiku wa tukio hilo la mauaji lakini hakuweza kutoka usiku huo ili kushuhudia nini kinaendelea.

Kamanda Zelothe alisema Marehemu alikuwa akiishi na babu na bibi yake hapo Kijijini na kwamba siku ya tukio walikuwa wameondoka kwenda katika Vijiji vya jirani, ambapo bibi yake na marehemu alikuwa amekwenda  Kongwa kwa ajili ya kujengea makaburi na babu yake alikwenda kijiji cha  Banyi banyi kwa Shughuli za kutemebelea wagonjwa.

Wakati huo huo Gari lenye namba za usajili T. 750 AEU aina ya TOYOTA CHASER likiendeshwa na Kenedy James mwenye umri wa miaka 48, Mkazi wa Mpwapwa liliacha njia na kupinduka na kusababisha kifo cha Salum Kaduma mwenye umri wa miaka (13) Mwanafunzi wa kidato cha kwanza Katika shule ye sekondari ya Mpwapwa, na kusababisha kifo chake. 

Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma alisema ajali hiyo ilitokea mnamo tarehe 12/08/2012 majira ya saa 09:00 asubuhi katika eneo la Kisima Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.

“Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa magurudumu mawili ya upande wa kulia kitu kilichopelekea gari hilo kuacha njia na kupinduka.” Aliongeza Bw. Zelothe

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate