Taarifa hii imepatikana via blogu ya Juma Mtanda, Morogoro.
Yafuatayo ni mahojiano ambayo aliwahi kuyafanya wakati wa uhai wake na HABEL CHIDAWALE huko Ddodoma.
Ni umbali wa kilomita 48 kutoka mjini Dodoma ukifuata Barabara ya Singida. Mita 50 pembeni mwa barabara hiyo upande wa mashariki, hapo ndipo ilipo nyumba anamoishi ombaomba maarufu nchini, Mzee Paulo Mawezi maarufu kwa jina la Matonya.
Yule Matonya aliyepata umaarufu jijini Dar es salaam na Morogoro kutokana na staili yake ya kuomba fedha kutoka kwa wapita njia. Ni Matonya aliyepata umaarufu zaidi baada ya mkuu wa zamani wa mkoa wa Dar es Salaam, Yusuf Makamba kumtimua jijini na kuagiza mamlaka husika kuhakikisha haruhusiwi kuingia kwenye mipaka ya Dar es Salaam. Ni yule ambaye baada ya kutimuliwa Dar es Salaam, aliibukia Morogoro ambako aliendeleza staili yake ya kuomba akiwa amelala chali huku mkono akiwa ameunyoosha juu kwa muda mredfu bila ya kutikisika hata kama jua ni kali kupita kiasi.
Kijijini, Matonya anaishi kwenye nyumba ya tembe ambayo ni mali ya mtoto wake wa kike aitwaye Elizabeth Matonya.

No comments:
Post a Comment