
Mmoja wa wasanii mahiri katika fani ya uigizaji hapa nchini, Wema
Sepetu akifanya mahojiano mafupi na Millard Ayo wa Clouds FM mapema leo
kwenye amsha amsha ya tamasha la Serengeti Fiesta ambalo linafanyika
jioni ya leo mpaka lyamba ndani ya uwanja wa chuo cha Ushirika,ndani ya
mji wa Moshi, ambapo katika tamasha hilo kiingilio kimepangwa kuwa ni
nusu mnyama tu a.k.a 5,000/= kwa kila kichwa.

Wema Sepetu pia akizungumzia ujio wao ndani ya mji wa Moshi, kuwa wao
kama Wasanii Nyota wa Filamu wamewasili mkoani humo kusaka vipaji vipya
mbalimbali vya filamu, usahili huo unafanyika kwenye ukumbi wa Mr Price,
ulioko mtaa wa Malindi.

Mtangazaji wa Clouds FM,Millard Ayo akiwa Live mapema leo mtaa wa
Malindi katika mpango mzima wa amsha amsha kwa wakazi wa Moshi kuhusiana
na tamasha la Serengeti Fiesta 2012, ambapo pia katika tamasha hilo
kutatolewa zawadi mbalimbali ikiwemo gari ndogo aina ya Vits kama
uinavyo pichani ikinadiwa vilivyo.

Kawa kawa amsha amsha ya tamasha la Serengeti Fiesta pia linatoa mafuta
kwa magari daladala,pikipiki sambamba na baji lita 10 ama tano kutoka
kampuni ya GAPCO ambao pia ni sehemu ya wadhamini wa tamasha hilo.

Msanii mwingine nyota katika tasnia ya filamu, Aunt Ezekiel akielezea
ni namna tamasha la Serengeti Fiesta lilivyowambamba wakazi wa mji wa
Moshi na vitongoji vyake, na pia ujio wao kuwatafuta wasanii wapya
chipukizi katika tasnia hiyo ambayo imekuwa ikikua siku hadi siku.

Wema Sepetu katika pozi na washabiki wake mapema mchana huu.

Mastaa wetu wa filamu hapa nchini, wametokelezeaje sasaaa.

Kiongozi wa msafara wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012, Mully B akiwa
na mastaa wa filamu, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel afu fulllll BBM kama
kawa.

Millard Ayo akifanya mahojiano na Ray a.k.a Vincent Kigosi kuhusiana na ujio wao ndani ya mji wa Moshi


Kutoka kushoto ni Mr Hatman, Steve Nyerere, Bonge pamoja na Millard Ayo katika 'shoo love' ya pamoja.

Wema Sepetu akijiweka sawa.

Wakiwa katika mazungumzo yao ya hapa na pale.

Kila mmoja ana haki ya kupata habari na kuhabarishwa.


Pichani ni Gari aina ya Vits itakayotolewa jioni ya leo kwenye tamasha
la Serengeti Fiesta 2012, kwa mshindi atakaejishindia kwenye droo
itakayofanyika katika uwanja wa chuo cha ushirika, ambako tamasha hilo
litarindima mpaka majogoo.

Jacob Steven a.k.a Steven akifafanua jambo mapema leo mtaa wa Malindi
kuhusiana na suala zima la wasanii hao kulivamia jiji la Moshi.

picha zote na: Ahmad Issa Michuzi
P.O BOX 4156, DAR ES SALAAM.
P.O BOX 4156, DAR ES SALAAM.
No comments:
Post a Comment