EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, August 17, 2012

Ni uhalifu mdogo usio na madhara" - Mmiliki wa shule Mwanafunzi aliyovuliwa nguo darasani

Mkazi wa Dar es Salaam aliyejitambulisha kuwa mmoja wa wamiliki wa shule ya Mtakatifu Benedict ya Dar es Salaam, amesema suala la mwalimu aliyehusika na suala la kuvua nguo wanafunzi darasani kama adhabu ni uhalifu wa kawaida usio na madhara kwa mtoto.

Akijitambulisha kwa jina la Renatus Michael, amesema uhalifu mkubwa ni wa kupiga wanafunzi viboko kama ambavyo imezoeleka kufanywa na baadhi ya walimu katika shule mbalimbali nchini.

Michael, ambaye alizungumza jana na gazeti hili kwa njia ya simu akidai kuwa Dar es Salaam, aliongeza kuwa uongozi wa shule una mpango wa kumchukulia hatua mwalimu aliyehusika na tukio hilo ambaye ni wa jinsi ya kike.

“Mimi nawashangaa sana mlivyoandika habari hiyo, hayo ni mambo ya shule na huo ni uhalifu mdogo usio na madhara kwa mtoto … ndiyo maana hata Polisi waliliweka pembeni, kwani limekaa muda wote huo … mmeandika kwa ukali kama vile lilikuwa suala la kupiga viboko?” Alihoji huku akilalamikia kuandikwa kwa taarifa hizo.

Alisema tukio hilo ambalo liliwakuta wanafunzi wanne wa kiume lilitokea Julai na mara kwa mara amekuwa na mazungumzo na mzazi aliyetoa taarifa hizo Polisi bila maafikiano.

“Ukweli ni kwamba tuliwahi kukaa naye sehemu mbalimbali na mara ya mwisho tulikutana usiku hotelini eneo la Buza ambapo mzazi huyo alikuwa akilalamika kwa nini mtoto wake afanyiwe kitendo hicho ambacho kingeweza kumwathiri kisaikolojia,” alisema Renatus.

Alisema akiwa mmiliki alijitahidi kumwomba radhi mzazi huyo akimhakikishia kuchukuliwa hatua dhidi ya mwalimu huyo, lakini hakutaka yaishe na ndipo alipotoa taarifa Polisi.

Kuhusu kuchukuliwa hatua mwalimu huyo, alisema uongozi wa shule una mpango wa kufanya hivyo na kwamba ulikuwa ukisubiri kuanza kwa likizo ya Septemba.

Kuhusu ni kwa nini uamuzi juu ya mwalimu huyo uchukue muda mrefu kiasi hicho ikilinganishwa na athari iliyowakuta wanafunzi hao, alisema kuna adhabu ya kumpa mwalimu na kuna adhabu ya wanafunzi, hivyo ni lazima uchunguzi wa suala hilo ukamilike.

Hata hivyo, Renatus alihofia kusambaratika kwa shule hiyo ambayo alidai ni changa ikiwa na wanafunzi pungufu ya 120, akisisitiza kuwa hata wao kitendo hicho hakikuwafurahisha.

via HabariLeo

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate