MCHEZA sinema wa Bongo aliye nyuma ya
nondo katika Gereza la Segerea, jijini Dar es Salaama kwa madai ya
kuhusika na kifo cha Msanii Steven Kanumba, Elizabeth Michael ‘Lulu’
amesema kuwa amepamisi sana uraiani.
Akizungumza na mwandishi wetu
Agosti 13, mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambako kesi
yake inaendelea kutajwa, Lulu alisema amemisi vitu vingi vya uraiani,
ikiwemo mitaa ya Sinza na Kinondoni alikozoea kwenda kujiachia, pia
anawakumbuka sana mashosti wake akina Diana Kimaro ‘Pacha wa Lulu’.
“Nimekumisi
sasa… (anataja jina la mwandishi), pia nimewamisi watu wote huko
uraiani, nimewamisi mashosti wangu jamani, nimemisi sehemu nilizokuwa
napenda kutembelea,“ alisema Lulu.
Lulu akionesha uso wa uchangamfu alisema anafurahi sana anapoona watu wanaofika mahakamani hapo ni baadhi ya marafiki zake na ndugu.
“Ukikaa kule (gerezani) unawakumbuka watu wengi, sasa ukija hapa (mahakamani) unapowaona watu mbalimbali unaowafahamu kidogo unafarijika, unakuwa mwenye amani siku hiyo,” alisema Lulu.

Kila Lakheri Lulu,Ata sisi mashabiki zako tumekumis pia,tena sana
tu.Mungu akufanyie wepesi uludi Uraiani ambapo naamini utakua mtu
tofauti sana na yle Lulu aliefahamika na wengi.

No comments:
Post a Comment