EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, August 16, 2012

Nitajiuzulu endapo itathibitika kuwa Chama kinatumiwa na CHADEMA

Kaimu Katibu Mkuu wa Chama Cha Walimu (CWT), Ezekiah Oluoch ametangaza kujiuzulu wadhifa wake ndani ya chama hicho iwapo Serikali itathibitisha kuwa kuna shinikizo la chama chochote cha siasa katika utendaji kazi wa viongozi wa chama hicho.

Kauli hiyo ya Oluoch imekuja siku kadhaa baada ya kuibuka tuhuma kuwa migomo inayoandaliwa na CWT kushinikiza walimu kudai nyongeza ya mshahara imekuwa na msukumo kutoka kwa vingozi wa CHADEMA.

Alidai tuhuma hizo tayari amezisikia kuwa yeye na Rais wa CWT wanashinikizwa na CHADEMA kuwataka walimu kugoma wakidai nyongeza ya mishahara yao, “Niko tayari kujiuzulu wadhifa wangu iwapo vyombo vya Dola vitabaini tumekuwa tukiwasiliana na viongozi wa CHADEMA katika kuanzisha hii migomo, wachunguze namba zangu za simu, utendaji wangu wa kazi na wanifuatilie kwa namna yoyote wakinithibitishia hata kidogo basi naachia ngazi,” alisema Oluoch.

Alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Rukwa baada ya ziara yake mikoani yenye lengo la kufanya tathmini ya mgomo wa walimu uliofanyika hivi karibuni kabla ya kuzuiwa na Mahakama Kuu kwa madai ya kukiukwa kwa kanuni na sheria kabla ya kutangazwa kwa mgomo huo.

Alisema mara kadhaa CWT inapotangaza kupambana na Serikali katika kudai haki za wanachama wake, kumekuwa kukiibuka maneno mengi huku viongozi wake wakituhumiwa kushinikizwa na viongozi wa chama fulani cha siasa jambo ambalo si la kweli, “CWT ni chama huru, hivyo kazi yake kubwa ni kuhakikisha maslahi ya wanachama yanatekelezwa lakini wanatimiza wajibu wao kwa Serikali, hivyo kutangaza mgomo ni haki yake na tulizingatia sheria ya Ajira na Mahusiano kazini ya mwaka 2004,” alisema.

Pia alisema CWT inakusudia kuwasilisha rufaa kwenye Mahakama ya Rufaa wiki ijayo, kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu inayoeleza kuwa mgomo wake uliotangazwa hivi karibuni ulikuwa batili.

Katika hukumu hiyo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iliamuru CWT kusitisha mgomo wa walimu walioutangaza kote nchini lakini pia wakitakiwa kulipa fidia kwa hasara zote zilizotokea wakati wa mgomo huo.

Alisema rufaa ya kupinga hukumu hiyo ilikuwa iwasilishwe mapema, lakini walikuwa wakisubiri Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuwasilisha hotuba ya Wizara yake bungeni ili wabunge wapate fursa ya kuchangia kwa upana, badala ya kuzuiwa kujadili kiundani.

Tulijua iwapo kesi hiyo ingekuwa imefunguliwa, Spika angewazuia wabunge kujadili kwa upana kwenye hotuba hiyo, hivyo wiki ijayo utakuwa ni wakati muafaka wa kufungua kesi ya kukata rufaa,” alisema.


No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate