EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, August 16, 2012

Wizara yataarifu kuhusu habari ya gazeti la Rai, "UCHIMBAJI WA URANI SERIKALI YAONYWA"

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

TAARIFA KWA UMMA 


Tarehe 16 Agosti, 2012 gazeti la Rai Toleo Na.986 katika ukurasa wake wa kwanza na watatu lilichapisha taarifa yenye kichwa cha habari “UCHIMBAJI WA URANI SERIKALI YAONYWA” na kuwa kumezuka sakata lingine ambapo kampuni ya kigeni  imeanza kuchimba madini hatari aina ya urani kwa kile wachunguzi wanasema ni kinyume cha sheria. Gazeti hilo liliendelea kuandika  kwamba Tanzania haina sera ya urani na kwamba hata kama Serikali imeruhusu uchimbaji huo, ni kinyume cha sheria kwa sababu hata Serikali yenyewe haijatunga sheria ya uchimbaji urani. Tunasema habari hii inamalengo ya kuupotosha umma.

Mwandishi wa habari hii bila ya kutaja jina lake anaeleza kuwa hakuweza kuwasiliana na viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini licha ya yeye kuwaandikia ujumbe kitu ambacho hakina ukweli. Kutokana na unyeti wa habari yenyewe mwandishi alipaswa kuhakikisha anapata taarifa kamili kutoka Wizarani na siyo kutoa taarifa kwa matakwa binafsi.

Habari hii imelenga zaidi katika kupotosha umma badala ya kuelimisha kama ambavyo mwandishi ameshindwa kueleza kwa ufasaha ni nini hasa kusudio lake. Tunaheshimu Uhuru wa vyombo vya Habari na tungependa kama kuna suala lolote linalohitaji ufafanuzi, Wizara ipo tayari muda wowote kutoa maelezo badala ya kukimbilia kuandika habari zinazojichanganya na kusababisha usumbufu kwa wananchi.

Tunatumia fursa hii kwa mara nyingine kuufahamisha umma kuwa kama Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini Mhe: Prof Sospeter Muhongo alivyosema kwenye hotuba ya bajeti ya mwaka huu kuwa pamoja na kuwepo kwa maeneo mbalimbali hapa nchini yenye madini ya urani ni maeneo mawili yaani Wilaya ya Namtumbo na Monyoni ndiyo yaliodhibitishwa kuwa na kiasi cha kutosha kuweza kuchimbwa kibiashara na si kweli kuwa uchimbaji umeanza.
Eneo la Namtumbo lipo ndani ya Hifadhi ya Taifa na Serikali iliwasilisha maombi UNESCO ya kurekebisha mipaka ya eneo la hifadhi ya Dunia ili kuongeza eneo la mradi, ombi liliridhiwa katika kikao cha UNESCO cha tarehe 02/Julai,2012 kilichofanyika Saint Petersburg (Urusi).

Aidha, Sera ya Madini ya Mwaka 2009 na Kanuni za Madini ya Mionzi Ayonisha za Mwaka 2010 - the Mining (Radioactive Minerals) Regulations, 2010 chini ya Sheria ya Madini, 2010 zinatumika katika kusimamia shughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini ya urani nchini. Sheria na Kanuni zote zilizotungwa na zitakazoendelea kutungwa zinazohusiana na usimamizi wa madini ya urani pamoja na mambo mengine zinalenga kuzingatia  miongozo/taratibu za Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA) za usimamizi wa madini hayo zinazohakikisha kuwa uchimbaji hauleti  athari kwa binadamu na mazingira.

Tunaendelea kuwashauri waandishi wa habari kuwa sisi kama wizara na chombo cha Serikali tunawajibu wa kuelimisha umma juu shughuli mbalimbali za wizara hivyo tunawashauri  kuwa tushirikiane kwa maslahi ya taifa badala ya kutoa habari zenye malengo binafsi.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Nishati na Madini

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate