Raia wa Indonesia, Mychel Takahindangeng (29), amekamatwa katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam
akisafirisha dawa za kulevya aina ya kokeni zenye thamani ya Shilingi
milioni 200.
Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa alisema Takahindangeng ambaye alikuwa na hati ya kusafiria yenye namba A2915930 ya Juni 7, mwaka huu, alikamatwa uwanjani hapo jana saa 9:45 alasiri akisafirisha unga huo kwa kuuhifadhi ndani ya begi la nguo.
Alisema mtu huyo aliyekuwa akisafiri kwenda Vietnam na ndege ya Oman Airlines, alikamatwa kwa ushirikiano mzuri wa askari polisi na watumishi wa uwanjani hapo akiwa na pakiti 4 za unga huo wenye uzito wa kilo nne, “Alikuwa anaelekea Vietnam kupeleka huu unga, lakini alikamatwa uwanja wa ndege, na ni kwa ushirikiano mzuri ambao upo baina yetu na watumishi wa uwanja wa ndege,” alisema Nzowa.
Aliongeza kuwa mtu huyo inaonekana ni mzoefu wa kusafirisha dawa za kulevya kutokana na maelezo yake kwani nchi alizotembelea hivi karibuni ni pamoja na China, India, Timor Mashariki na Tanzania, “Inaelekea ni mzoefu kwa sababu kutokana na maelezo yake inaonekana hata hizi nchi alizotembelea hivi karibuni alikuwa akisafirisha madawa,” alisema Kamanda Nzowa na kuongeza kuwa upelelezi ukikamilika, atafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.
Hata hivyo, Nzowa aliwashukuru baadhi ya raia wema ambao wamekuwa wepesi kutoa taarifa na hiyo yote ni kutokana na elimu ya upigaji vita wa dawa za kulevya wanayojitahidi kuitoa.
via HabariLeo

No comments:
Post a Comment