Leo
mchana kumetokea purukushani na vurugu katika mji wa Kigamboni eneo la
Kisota kwa sababu wananchi wanaojishughulisha na uchimbaji kokoto
walizuiliwa na Serikali kuendelea na shuguli hiyo.
Wananchi waliokuwa na ghadhabu walifunga barabra kwa mawe na kuwasha matairi barabarani kama inavyoonekana pichani.
Inaripotiwa askari wa kuzuia fujo, FFU, walikuwa katika eneo husika ili kutuliza ghasia na kurejesha usalama wa raia na mali.

(picha via ukurasa wa facebook wa Dkt. Mkunde Mlay)
Askari
wa Kikosi cha Kutuliza ghasia (FFU), wakiwa wameweka doria katika
barabara kuu ya kutoka Kigamboni kwenda Mji Mwema Dar es Salaam leo,
baada ya kudhibiti vurugu za wachimba kokoto wa eneo la Maweni ambao
walifunga barabara hiyo kwa mawe kwa zaidi ya masaa natatu na kuchoma
matairi wakishinikiza kuruhusiwa kuchimba kokoto. (picha: RICHARD
MWAIKENDA)
Baadhi
ya mawe yaliyoondolewa barabarani baada ya kuwekwa na wachimba kokoto
eneo la Maweni, Kigamboni. Watu kadhaa wanaotuhumiwa kufanya vurugu hizo
wametiwa mbaroni. (picha: RICHARD MWAIKENDA)
No comments:
Post a Comment