Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Askofu Mstaafu wa Jimbo la Dodoma,
Mhahamu Mathia Isuja wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wa kijiji
cha matumaini cha Dodoma kinacholea watoto yatima. Mheshimiwa Pinda
alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za miaka 10 ya kijiji hicho. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Serikali imesema kuwa itaangalia namna
ya kuviwezesha vituo vya kulelea watoto yatima, wenye matatizo ya kiafya
hasa wale walioathirika na virusi vya UKIMWI ili viweze kupatiwa ruzuku
ya kuweza kusaidia katika matibabu ya watoto hao.
Hayo yalisemwa jana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwenye maadhimisho ya miaka 10 ya Kijiji cha Matumaini kilichopo Manispaa ya Dodoma ambacho kinamilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Dodoma.
Alisema Serikali imekuwa ikifanya jitihada za kuhakikisha inapunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano na katika bara la Afrika kwenye nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara, Tanzania inaongoza, “Serikali itaendelea kusaidia upatikanaji wa dawa za kuongeza siku za kuishi ambazo tunaelewa ni za gharama kubwa, aidha mapungufu yanayotokana na watendaji wa Serikali tutajizatiti katika kurekebisha hayo,” alisema.
Aidha alisema, hakuna sababu za kuchelewa kwa hundi ya Hazina kwenye Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), hatua ambayo husababisha watoto kukosa dawa na lishe.
Alisema kuwa, wameanza kutafuta ufumbuzi wa kuwa na mfumo mzuri wa kutoa makontena yenye misamaha ya kodi kwa wakati ili kuweza kupunguza gharama kwa wahusika.
Alisema kuanzishwa kwa kituo hicho kumeongeza matumaini ya kuishi na kuwapa uhakika na usalama wa maisha yao ya sasa na siku za usoni kwa watoto wengi ambao walikuwa wamepoteza matumaini.
Waziri Mkuu alisema kuwepo kwa kituo hicho kumewasaidia wengi kupata elimu kuanzia ngazi ya awali hadi sekondari.Awali, Askofu Mathias Isuja, alitaka jamii isidharau watoto na badala yake watoto walelewe katika malezi mema yanayompendeza Mungu.
Akisoma risala, Sista Teresia, aliomba Serikali kuangalia namna ya kuwapatia ruzuku kwa ajili ya kuweza kusaidia watoto wagonjwa ambao wamekuwa wakipatiwa dawa za kurefusha maisha. Alisema kituo hicho kinahudumia watoto 160 ambao wanaishi kwenye familia 13 na mpaka sasa nyumba zilizokamilika ni nane.
---
via HabariLeo

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Sister Rosaria ambaye ni
mwanzilishi wa Kituo cha kulelea watoto yatima kiitwacho kijiji cha
matumaini cha Dodoma, wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 10 ya kituo
hicho.
No comments:
Post a Comment