
NGULI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond
Platinum’ amebainisha hisia zake kuwa endapo akimshirikisha msanii
mwingine katika kazi zake “collaboration’, anaamini hazitafanya vizuri
ukilinganisha na akiimba mwenyewe.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam juzi, Diamond
alisema, kichwani kwake kuna mashairi yasiyo na idadi, ambayo kila siku
yanaongeza, hivyo haoni sababu ya kumshirikisha msanii mwingine katika
kazi zake.
“Mimi mwenyewe sielewi, nitakuwa nahitaji nini kwa huyo nitakaye
muomba nimshirikishe, naamini nitamsumbua, maana mwisho wa siku nitaona
kama ananiharibia, kiukweli najiamni sana na sitarajii kumshirikisha
msanii yoyote wa bongo katika kazi yangu,” alisema.
Diamond, kwa sasa yupo kwenye mchakato wa kuandaa video ya wimbo wake
unaokwenda kwa jina la
‘Usiniumize’ ambao unafanya vizuri katika vituo
mbalimbali vya redio.
Mbali na kibao hicho, Diamond alishawahi kutamba na vibao vyake kama,
‘Mawazo’, ‘Moyo wangu’, ‘Nimpende Nani’ na nyinginezo, ambazo
zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki wa kizazi
kipya nchini.
Habari na Elizabeth John
No comments:
Post a Comment