Mwalimu Brailsford anasema Uingereza inatakiwa kukaza kamba kwa
kuhakikisha hawapotezi kanuni walizotumia kufikia hesabu nzuri ya jumla
iliyowaweka juu kiasi hicho – nafasi ya tatu kwa ujumla.
“Mambo yamekwenda vizuri, ugharimiaji umeleta tofauti kubwa katika jinsi nchi ilivyofanya vizuri kwenye michezo. Inaendeshwa na kusimamiwa vizuri. Inafanya kazi. “Kinachonitatiza kidogo ni hili suala la kutaka kubadilisha mfumo. Wanakuja watu wanataka kuanza mambo upya kwa mawazo tofauti katika kila kitu,” anasema.
Maoni yake ni kwamba njia ambazo Uingereza imeanza kufuata zinatakiwa kuenziwa. Hataki kuona wanasiasa wakiingilia kuelekeza cha kufanya, wakati tayari mafanikio yameanza kuonekana. Badala yake, anaona dalili za mafanikio zaidi zitatokana na vyama vya michezo tofauti kushindana katika kila kimoja kujaribu kuongoza michezo kisomi.
“Kwa kifupi ni kwamba mfumo huu unafanya kazi, tusipouingilia na kuuvuruga, utaendelea kufanya kazi. “Huwezi kuwekeza kwenye michezo kama tunavyofanya uache kufanikiwa… mbaya ni kugutuka na kufanya mabadiliko yasiyo na msingi. Kwa hiyo wanasiasa kaeni mbali, elekezeni fedh kwenye michezo, ziende kwa wakurugenzi,” anasisitiza.
Kwa watakaosikiliza ushauri bila shaka wataona mafanikio, kama aliyowezesha Brailsford kwenye Michezo ya 30 ya Olimpiki.
Mmoja wa chipukizi, kijana mwenye umri wa miaka 18 – Katie Kirk, alikuwa kwenye timu iliyopata ushindi wa kwanza katika mbio za kupokezana vijiti katika michuano ya Ubingwa wa Ulaya mwaka jana. Sasa amenuia, na yupo katika mipango ya kuhamia kwenye mbio za mita 800 kwa ajili ya michezo ijayo ya Olimpiki.
Katie anayetoka Belfast, anasema kwamba mfano uliowekwa na wana Team GB waliopata medali ni hamasa tosha kwake kufanya kazi kwa nguvu zaidi kulifikia lengo lake, “Hii inakuhamasisha kuongeza jitihada kwa sababu unajua unataka uwepo na ushindane katika ngazi hiyo.“Medali zote zilizopatikana zina maana kubwa mno, kwa sababu ukifuatilia waliozipata, utaona jinsi walivyokuwa wakipiga hatua moja baada ya nyingine. “Nakumbuka kumtazaa Mo Farah miaka michache iliyopita, alikuwa akikimbia vyema lakini hakuwa vizuri kama alivyo leo. Hii inaonesha kwamba ukiongeza bidii utafikia ngazi unayotaka,” anasema binti huyo.
Katie alichaguliwa na Dame Mary Peters, mwanariadha pekee alyepata medali ya dhahabu katika Olimpiki ya mwaka 1972 iliyofanyika Munich. Mchezo alioshindia dhahabu, leo hii hujumuisha hatua mbalimbali, zikiwamo riadha, kuruka na kulenga shabaha. Ndio mchezo alioshinda Jessica Ennis.
“Nilikuwa na kocha mmoja, aliyezoea kukandamiza mkono wangu kwa nguvu huku akisema; ‘umefanya vyema, lakini ungeweza kufanya vizuri zaidi’. “Lakini leo wachezaji wana wataalamu wa saikolojia, wana wataalamu wa mifumo ya kibayolojia…kila aina ya wataalamu kwenye masuala ya afya, tofauti kabisa na enzi zetu,” anasema Peters.
“Ukipata watoto katika miaka yao ya awali – China wanawaanzia katika umri wa miaka mitatu – unaweza kuwajenga kuwa mabingwa. “Lakini si kila mtu anataka kufuata njia hiyo, wengine wanataka kuwa na nyakati nyingi za kupumzika na furaha zaidi.“Hata hivyo, hakuna jambo la furaha zaidi ya unavyojisikia baada ya kushinda, umesimama kwenye jukwaa na unasikiliza wimbo wa taifa unapigwa,” anatoboa siri hiyo.

No comments:
Post a Comment