Bi. Harriet Macha kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC)
akizungumza na mtandao wa vikundi vya vijana kata ya Kibada -Kigamboni
akiwaeleza jinsi Umoja wa Mataifa unavyohusika katika maendeleo ya
vijana ikiwemo kuwaelimisha haki zao, kuwawezesha kujitambua na kujua
umuhimu na kazi za mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini.
Naibu Mwenyekiti wa kikundi cha vijana kata ya Kibada akizungumzia
changamoto zinazowakabili kama kikundi ikiwemo ukosefu wa maktaba ambazo
zingewawezesha kusoma na kujua mashirika hayo yanafanyaje. Pia tatizo
lingine ni jeshi la polisi kuwafikiria na sheria zake ikiwemo kuwapangia
muda wa kutembea, kukithiriri kwa rushwa mambo ambayo yanachangia
kuongeza uduni wa maisha ya vijana.
Mmoja wa mwanakikundi wa vijana kata ya Kibada-Kigamboni mwenye kipaji
cha kuigiza akionyesha uwezo wake wa kuigiza ikiwemo jinsi vijana
wanavyokwamishwa kuanzia kwenye sekta ya elimu na kujiajiri na hata
hivyo Bi. Harriet Macha wa UNIC alitoa ushauri jinsi ambavyo Shirika
hilo linavyofanya kazi na serikali na mipaka yake.
Mwanakikundi wa kata ya Kibada Kigamboni akielezea kipaji chake cha
ususi kilichompelekea kujiajiri na kujitegemea na kuahidi kutoa mafunzo
kwa wasichana wenzake.
Pichani Juu na Chini ni Bi. Harriet Macha kutoka Kitengo cha Habari cha
Umoja wa Mataifa (UNIC) akizungumza na vijana Somangile-Kigamboni
kutoka kikundi cha 'Kigamboni Peer Educator Network' (KIPENET) kuhusiana
na kazi za shirika hilo na huku akipokea changamoto kutoka kwao.
Mwenyekiti wa vijana wa KIPENET Sagara Msumi akitoa tathmini ya
mafanikio yao tangu waanze kufanya kazi na UN yanaonekana kufuatia
kupungua kwa matukio ya mimba za utotoni kutokana na kusambaza vijarida
vinavyotolewa na umoja wa Mataifa.
Wanawake wa kikundi cha 'Save The Women Tanzania' wakitoa burudani ya
uigizaji wanayotumia kutoa elimu kwa jamii mbele ya mwakilishi kutoka
kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (hayupo pichani).
Katibu wa kikundi hicho Mtupeni Saidi akifafanua hatua waliofikia
katika kuelimisha vijana wenzao hususan wanawake katika kupanga uzazi,
kupiga vita mimba za utotoni na kuliomba Shirika la Umoja wa Mataifa
kuendelea kuwaunga mkono kwa njia ya kufanya matamasha na kuzunguka
katika shule tofauti.
Mweka hazina wa kikundi cha vijana cha KIPENET, Swaka Abbas akitoa yake
machache ambapo ameuomba Umoja wa Matifa kuwaboreshea maktaba yao na
kuwaongezea semina za kuwaelimisha.
Kikundi cha vijana cha KIPENET kikimba nyimbo za kuishukuru UN kwa kuwaonyesha Mwanga wa Maisha na Maendeleo.
Picha & maelezo: Zainul A. Mzige, Operation Manager, MO BLOG,
No comments:
Post a Comment