EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, August 13, 2012

Utoroshwaji wa wanyama pori: Taarifa ya Wizara ya Kuwatimua kazi; Kuwapa onyo Wafanyakazi

Picture: Khamis Kagasheki
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uamuzi wa Serikali wa kuwafukuza kazi watumishi watatu wa wizara hiyo kutoka na ukiukaji wa sheria na utekelezaji wa majukumu yao ya kazi kufuatia sakata la usafirishaji wa wanyama pori kupitia Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kwenda Quatar. (picha: Picha na Anna Nkinda – Maelezo)

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

HATUA ILIYOCHUKULIWA KUHUSIANA NA UTOROSHWAJI WA WANYAMAPORI K.I.A.
 


Wizara ya Maliasili na Utalii imechukua  hatua za kinidhamu kwa watumishi wake tisa (9)  kufuatia kadhia ya utoroshaji wa Wanyamapori Hai katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na masuala mengine yanayohusu Wanyamapori. Watumishi hao wamechukuliwa  hatua husika kufuatia kukamilika kwa uchunguzi wa tuhuma zilizokuwa zikiwakabili.

(1)   Waliofukuzwa kazikutokana na ukiukaji wa sheria katika utekelezaji wa majukumu yao ni:

(i)       Bw. Obeid F. Mbangwa - Mkurugenzi wa Wanyamapori. Wakati wa kadhia hiyo alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Matumizi
          ya Wanyamapori,
(ii)      Bw. Simon Charles Gwera  – Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii – CITES na Utalii wa Picha Arusha,
(iii)     Bw Frank Mremi - Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii – CITES na Utalii wa Picha Arusha.

(2)  Aliyeondolewa Cheo cha Madaraka kutokana na kutochukua hatua kamilifu za ulinzi ambazo zingeweza kuzuia kutokea
       kwa tukio la utoroshwaji wa wanyama ni:

(i)         Bw. Bonaventura M.C. Midala – Mkurugenzi Msaidizi, Undelezaji Wanyamapori.  Wakati wa tukio alikuwa Mkurugenzi
            Msaidizi Sehemu ya Kuzuia Ujangili.

(3)  Wafuatao ni Maafisa Wanyamapori Daraja la II waliotekeleza maelekezo ya Wakuu wao wa kazi yaliyo kinyume cha Sheria ambao wamepewa Onyo Kali la Maandishi:

(i)        Bibi Martha P. Msemo - Afisa Leseni, Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Arusha.
(ii)       Bibi Anthonia Anthony – Afisa Leseni, Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Dar es Salaam.

(4)   Bw. Silvanus Atete Okudo ni Mkuu wa Kituo cha Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Arusha aliyeshindwa kufuatilia kupata maelekezo ya Mkurungezi wa Wanyamapori kuhusu mtumishi wake aliyekiuka Sheria katika utoaji wa vibali.  Aidha, alishindwa kupeleka kwa Katibu Mkuu taarifa kuhusu mtumishi huyo ili achukuliwe hatua za nidhamu.

(i)         Silvanus Atete Okudo – amepewa Onyo Kali la Maandishi.

(5)  Wafuatao ni Maafisa ambao uchunguzi dhidi yao unaendelea:

(i)        Bw. Mohamed Madehele – Ofisi ya Matumizi Endelevu ya Wanyamapori
(ii)       Bibi Mariam Nyallu – Kituo cha Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha – Arusha.

Wahusika wengine katika kadhia hiyo wasiokuwa waajiriwa wa Wizara ya Maliasili na Utalii  watachukiliwa hatua na mamlaka nyingine husika.

[MWISHO]
Mhe. Khamis Suedi Kagasheki
WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII
13 Agosti 2012

(Imetolewa kwenye Press Conference iliyofanyika Viwanja nya Bunge Dododma Dodoma tarehe 13 Agosti 2012)

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate