EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, August 13, 2012

JACK CHUZ ABONDWA NA MWANAUME


Stori: Richard Bukos
STAA wa sinema za Kibongo, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ anadaiwa kubondwa na mwanaume mmoja mwigizaji aitwaye Mandela Nicholaus a.k.a Jacob, hivyo kulazimika kukimbilia Kituo cha Polisi cha Pangani, Ilala jijini Dar es Salaam kuokoa maisha yake, Ijumaa Wikienda lina mkasa kamili.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kilichokuwa eneo la tukio, sakata hilo la aina yake lilitokea kwenye Hoteli ya Lamada, Ilala, Dar mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo Jack Chuz na waigizaji wenzake walikuwa wameweka kambi kwa ajili ya kurekodi filamu.

Chanzo hicho kilidai kuwa Jacob alimuuzia Jack Chuz muswada wa filamu (script) na kukubaliana kuwa ataiongoza lakini kabla ya kumaliza kazi hiyo, muongozaji huyo alidai kuwa waigizaji aliokuwa akiwaongoza walikuwa wakimfanyia dharau hivyo kusitisha zoezi hilo.
Chanzo hicho kilitiririka kuwa baada ya kusitisha zoezi hilo, Jacob alimtaka Jack Chuz amrudishie chake kwani alikuwa amempatia Sh. milioni 1.4 lakini sistaduu huyo alisema hawezi kumpa fedha hizo ndipo likaibuka varangati zito hotelini hapo.

Ilisemekana kuwa mtiti huo ulitawaliwa na ngumi na mateke ya judo, hali iliyosababisha kuibuka kwa mayowe na vilio vya kuomba msaada kabla ya baadhi ya wasanii waliokuwa na Jack Chuz, Slim Omary, Mary Mtema na mpiga picha wao, Mohammed Kibinda kumnasua staa huyo ambaye alitoka nduki hadi Kituo cha Polisi cha Pangani, Ilala na kufungua jalada la kesi namba ILA/RB/3042/12 -SHAMBULIO.
Ijumaa Wikienda lilifika kituoni hapo na kuwakuta wawili hao ambapo Jacob alisema anamdai Jack Chuz Sh. milioni 1.4 kwa ajili ya kumuuzia script ya filamu hiyo pamoja na kumuongozea kabla ya kutokea mtafaruku.
Kwa upande wake, Jack Chuz aliliambia gazeti hili kuwa anachoweza kumlipa ni shilingi laki tano na si zaidi ya hapo kwa kuwa ‘dairekta’ huyo alitaka kumkomoa kwani hamdai kiasi hicho.
Paparazi wetu aliwaacha wawili hao wakiwa kwenye harakati za kutaka kuburuzana kortini.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate