Baada ya kufahamu hivyo nikawa na kiu ya kutaka kujua ni lini tutaanza kumuona akichekesha tena ndani ya Orijino Komedi hivyo nikapata nafasi ya kuzungumza na Wakuvanga ambae ndio mkurugenzi wa kampuni inayoisimamia Orijino Komedi.Namkariri akisema “ukweli niwe muwazi, kwa afya yake na tatizo alilonalo tunazungumzia tatizo la mshipa wa fahamu, tunazungumzia kitu kinaitwa ubongo, hayo matatizo yanachukua muda mrefu sana ukizungumza ukiwaambia watanzania kwamba atarudi hivi karibuni unakua unajidanganya wewe na watanzania wenzio, ndio maana siku zote tunasema ukiwa na nafasi ya kumuombea mtu unaempenda muombee, mi siwezi kuahidi kwamba labda atarudi mwezi ujao au mwaka ujao”
Kuhusu kutafuta mtu wa kuziba nafasi ya Vengu, Wakuvanga amesema “tutaendelea kuwa na jina la Vengu maisha yote ya Komedi, kwetu sisi iko tofauti kidogo sisi tumeapa.. ndivyo tunavyoishi, tuko saba mpaka tunakufa.. kuongezeka kwa mtu labda sisi tukae pembeni tuwatafute watu wengine lakini tutaendelea kuwa saba, hata maeneo tunayoishi na jinsi tunavyoishi mara nyingi tunaishi tuko saba, akipungua mmoja bado tuko saba”
No comments:
Post a Comment