Wiki hii Twanga Pepeta itaendelea kukonga nyoyo za mashabiki wake kama kawaida katika kumbi za Club Billicanas siku ya Jumatano, Alhamisi watakuwa New Club Maisha Oysterbay, Ijumaa watakuwa Free Time Resort Ukonga, Jumamosi watakuwa Mango Garden Kinondoni na Jumapili watamalizia kwa onyesho la mchana Leaders Club Kinondoni na usiku watakuwa Mzalendo Club Millenium Tower.
Baadhi ya wasanii wa African Stars “Twanga Pepeta”.
Wakali wa Muziki wa Dansi wa hapa Bongo, African Stars “Twanga Pepeta” wamerejea jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yao ya maonyesho katika mikoa ya Iringa na Mbeya.
Ziara hiyo ilikuwa ni ya siku tatu kuanzia siku ya Ijumaa tarehe 14-09-2012, Jumamosi tarehe 15-09-2012 na Jumapili 16-09-2012 ambayo ilisababisha Bendi kutokufanya maonyesho katika siku hizo kama ilivyokuwa kawaida ya Twanga Pepeta.
Pia kwa wiki hii Bendi inataraji kuitambulisha nyimbo mpya ya Badi Bakule inayoenda kwa jina la “Mwenda Pole Hajikwai” ambayo itakuwa ni nyimbo mpya ya SITA ya Twanga Pepeta mara baada ya kuzindua albamu ya 11 ya DUNIA DARAJA.
Nyimbo nyingine mpya ni “Shamba la Twanga” iliyotungwa na Grayson Semsekwa,” Walimwengu hawana jema” uliotungwa na Jumanne Said au J4 lapova, “Mapambano ya Kipato” iliyotungwa na Mwinjuma Muumini, “Ngumu Kumeza” ya Mirinda Nyeusi na “Nyumbani ni Nyumbani” iliyotungwa na Kalala Jr.
HASSAN REHANI
MENEJA ASE
No comments:
Post a Comment