Sehemu ya umati wa watu wanaoendelea kuingia ndani ya uwanja wa Samora kujiachia kwa pamoja ndani ya muonekano mpya wa Serengeti Fiesta 2012.
Msanii wa filamu pia ni muigizaji wa filamu,Shilole akiserebuka jukwaani.
Aunt Ezekiel nae hakuwa nyuma kuachia mbwembwe zake kama kwa
|
Mkali wa hip hop ndani ya Bongofleva,Roma Mkatoliki akiwarusha vilivyo wakazi wa mji wa Iringa waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta ndani ya uwanja wa Samora. |
|
Ilikuwa ni ya kuvutia sana usiku huu ndani ya uwanja wa Samora,pale wasanii wa THT,Amin na Linah walipopanda jukwaani na kulishambulia vilivyo bila hiyana jukwaa la Serengeti Fiesta 2012,wasanii hao ambao ilielezwa kuwa walikuwa wapenzi baadaye ikadaiwa wameachana kila mmoja akawa anakamua muziki kivyake. |
|
Anaitwa Linah kutoka nyumba ya vipaji,THT,Linah akiimba wimbo wake Yalaiti. |
|
Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT,Amin akiimba jukwaani usiku huu mbele ya umati mkubwa wa watu waliojitokeza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012. |
Mkali wa miondoko laini katika anga ya muziki wa bongofleva,Ben Paul akiimba kwa hisia jukwaani mbele ya wakazi kibao wa mji wa Iringa na vitongoji vyake,ndani ya uwanja wa Samora,kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2012.
|
Sehemu ya wakazi wa Iringa wakishangweka vilivyo ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
|
Msanii mwingine chipukizi kutoka THT akiimba kwa hisia jukwaani . |
|
|
Msanii Recho akikamua jukwaani. |
|
Anaitwa Recho kutoka THT,kaiimba wimbo wake wa upepo mbele ya umati wa watu waliojitokeza kwa wingi (hawapo pichani) kwenye tamasha la serengeti fiesta linaloendelea hivi sasa kwenye uwanja wa samora mkoani Iringa. |
|
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Linex akiiimba kwa hisia jukwaani kwenye tamasha la serengeti fiesta 2012 |
Mmoja wa wasanii chipukizi aliyeibukia kwenye shindano la Serengeti Supa Nyota 2012,kutoka Mkoani Mbeya aitwaye Ney Lee pichani akionesha kipaji chake cha kuimba jukwaani kwenye uwanja wa Samora,mkoani Iringa ambako hivi sasa kunarindima tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Sehemu ya wakazi wa Iringa na vitongoji vyake wakishangweka kwenye muonekano mpya wa tamasha la serengeti fiesta 2012 ndani ya uwanja wa samora.
Ni mkali mwingine kutoka Morogoro kupitia shindano la Serengeti Supa Nyota 2012,Jo Maker akikamua vilivyo mbele ya wakazi wa mji wa Iringa wanaonelea kuingia hivi sasa ndani ya uwanja wa samora,kutibwirika pamoja na muonekano mpya wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Sehemu ya umati wa watu wanaoendelea kuingia ndani ya uwanja wa Samora kujiachia kwa pamoja ndani ya muonekano mpya wa Serengeti Fiesta 2012.
Ni mkali mwingine kutoka jijini Mwanza kupitia shindano la Serengeti Supa Nyota 2012, Young KIller akikamua vilivyo mbele ya wakazi wa mji wa Iringa wanaondelea kutinga hivi sasa ndani ya uwanja wa samora,kutibwirika pamoja na muonekano mpya wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
No comments:
Post a Comment