EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, September 18, 2012

KESI YA LULU, JAJI AWAHOJI MAWAKILI MMEILETA KESI HII MAHAKAMA YA RUFANI ILI IWEJE?

Elizabeth Michael
MAPITIO ya maombi ya utata wa umri wa msanii wa filamu Elizabeth Michael maarufu kama Lulu (18), anayekabiliwa na shtaka la mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba (28), jana yalichukua sura mpya baada ya jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani Tanzania kuhoji mawakili wa pande zote kwanini wamelifikisha suala hilo mahakama hapo badala ya kusubiri usikilizwaji wa awali.


Jopo la majaji watatu liliketi jana wakiongozwa na Mwenyekiti Jaji,  January Msoffe, Bernard Luanda na Edward Rutakangwa saa 3:00 walianza kuuhoji upande wa Jamhuri kwa sababu gani wameomba mahakama hiyo ifanye mapitio.


Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi  Faraja Nchimbi akisaidiana na Wakili wa Serikali Shadrack Kimaro,  ulidai kuwa umeomba mapitio kwa sababu uamuzi uliotolewa na Jaji Dr. Fauz Twaib alikiri maombi ya utetezi hayakuwasilishwa mahakamani kihalali kwa mujibu wa sheria.

Alidai kuwa, Jaji Dk. Twaib alitakiwa kuyaondoa  maombi hayo lakini badala yake alikubali kuyasikiliza ilhali alibaini kuwa hayako sahihi.

“Jaji Dk. Twaib alikosea kutoa tafsiri ya kifungu cha 44 (1) cha sheria ya mahakimu alipaswa kutoa maelekezo kwa mahakama ya Kisutu kulingana na makosa aliyoyaona katika uamuzi wa Hakimu Mkazi Augustina Mmbando na siyo kuyasikiliza yeye mwenyewe… tumeamua kuomba mapitio ili yasikilizwe haraka badala ya kukata rufaa,” alidai Nchimbi.

Alifafanua kwamba msingi wa malalamiko yao mahakamani hapo ni kuhusu uamuzi uliotolewa na Jaji Dk. Twaib ulikuwa na dosari kwa kuzingatia bado hoja ya msingi ilikuwa pembeni.

Jaji Msofe aliuhoji upande wa utetezi kwanini shauri hilo limefika Mahakama Kuu Tanzania, wakati Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji na kwa sababu gani wasingesubiri shauri lianze kusikilizwa katika usikilizwaji wa awali mahakama kuu baada ya upelelezi kukamilika.

Akijibu hoja hizo, wakili wa utetezi Peter Kibatala alidai kuwa  waliwasilisha maombi yao kwa sababu ya kulinda maslahi ya mtoto (mshtakiwa).

Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano kati ya jopo la majaji na wakili Kibatala;

Jaji Msofe: Kwanini mmelizungusha kote huku suala la umri wakati lingeweza kutazamwa katika usikilizwaji wa awali utakapoanza mahakama kuu au mngeweza kuipa nafasi kesi ikaendelea kule Mahakama ya Kisutu ambako ingekuwa imeshapiga hatua mbele sasa lakini kama mnapoteza muda kutaka utata wa umri usikilizwe ili iweje?

Kibatala: Watukufu Majaji, lengo letu ni kulinda maslahi ya mtoto (mshtakiwa) hii ni kesi ya mauaji ni lazima kuwe na namna ya kuweka kumbukumbu wakati wa ushahidi wake.

Jaji Msofe: Najisikia vibaya leo hii kukaona katoto kamekaa pale kizimbani. Huu ubishi wa kesi hii ya mauaji inayomkabili mshtakiwa, kuhusu umri ili iweje?

Kibatala: Hatukuwa na namna ya kuingiza ushahidi wa umri isipokuwa kwa kuomba mahakama ichunguze umri ili itakapofikia usikilizwaji wa kesi ya msingi iweze kuwa na kumbukumbu sahihi.

Jaji Luanda: Huyu sio mtoto wa kwanza kushtakiwa kwa kesi ya mauaji. Kifungu cha 26 cha kanuni ya adhabu lazima kiangalie adhabu ya mtoto anayekabiliwa na kesi kama hii labda mngeweza kutuambia kwamba Lulu hawezi kushtakiwa mnatuambia umri wake  ili iweje?

Kibatala: Tutaondoa shauri kwa ajili ya kurejesha Mahakama ya Kisutu ili kuendelea na usikilizwaji wa awali kabla upelelezi haujakamilika na kuhamishiwa Mahakama Kuu kwa ajili ya usikilizwaji wa kesi ya msingi.

Mwenyekiti wa jopo hilo, Jaji Msofe alisema watakwenda kutafakari hoja zilizotolewa na pande zote mbili ambapo watazijulisha pande hizo tarehe ya hukumu kama kesi hiyo iendelee kusikilizwa utata wa umri Mahakama Kuu ama jalada lirejeshwe Mahakama ya Kisutu kwa ajili ya usikilizwaji wa awali.

Mbali na Wakili Kibatala, mawakili wengine wa utetezi ni Kennedy Fungamtama na Fuljence Massawe ambapo waliwasilisha maombi mahakama kuu wakidai kuwa Lulu ana umri wa miaka (17) na siyo miaka (18) kama ilivyoandikwa kwenye hati ya mashtaka.

Katika kesi hiyo, Lulu anadaiwa kuwa  Aprili 7, mwaka Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alimuua Kanumba.

Aidha, kwa mujibu wa Mwenendo wa Sheria ya Makosa ya Jinai (CPA), Lulu hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji lakini mara upelelezi wake utakapokamilika itahamishiwa Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate