Ujumbe huu umekuwa-cross posted kutoka kwenye tovuti ya SHAFFIH DAUDA - shaffihdauda.com ambaye anasema:-
Mchana wa jana nikiwa safarini kurudi jijini Dar es Salaam nikitokea mkoani Singida, nilipokea barua pepe kutoka mwanaharakati na mwanariadha Wilhelm Gidabuday iliyokuwa ikielezea namna baadhi ya viongozi wanavyotumia madaraka yao vibaya ndani ya nchi hii inayoongozwa na utawala wa sheria.
Email aliyonitumia Gidabuday anaanza kwa kunitoa woga kwamba niiweke barua pepe yake kama ilivyo na kwani ana ushahidi wa kila alichoandika.
Barua pepe imeandikwa kama ifuatavyo:
MICHEZO, MISITU NA VYANZO VYA MAJI VINAPOHUJUMIWA KWA WAKATI MOJA NA VIONGOZI WALIOCHAGULIWA AMA KUTEULIWA ILI KUVILINDA!
1). Inawezekana vipi mbunge mzima wa wilaya ya Hanang awakingie kifua wajomba zake waliovamia viwanya vya michezo na vyanzo vya maji kwa wakati mmoja na wasichukuliwe hatua za kisheria hadi leo?
2). Kama hiyo haitoshi wananchi wa kitongoji cha Endamanang kijiji cha Nangwa walipofanya jitihada za kumweleza DC-Hanang na kufanikiwa kuwekwa ILANI YA SERIKALI lakini wajomba hao wa Mary Nagu wanaoitwa NINO YAHHI na SIKUKU AXWESSO wakavunja na kutupa ilani hiyo July19, 2011 na kuendelea kukingiwa kifua hadi leo huku wakiendelea kulima
eneo lililokatazwa kisheria hawajafunguliwa mashtaka hadi leo?
3). Je uvamizi wa viwanja vilivyoachwa na serikali yetu kwa manufaa ya watoto wetu, na uvamizi wa vyanzo vyetu vya maji ndiyo ilani ya CCM?Kama siyo ilani ya CCM basi haraka sana kabla ya uchaguzi wa CCM Mary Nagu awe wa kwanza kuwasihi wajomba zake kuirudisha ILANI YA SERIKALI pale palipowekwa na serikali ya wilaya March 13,2011, na pia yeye awe wa kwanza kama mbunge na mwana CCM wa kweli kuwatimua wajomba zake katika BONDE LA ENDAMANANG AMBALO NI VYANZO VYA MAJI VILIVYOPO KTK HIFADHI YA MLIMA HANANG, AMBAYO PIA ILIKUWA "RECREATIONAL AREA YA MAPUMZIKO YA WATOTO WA KIJIJI CHA NANGWA; Siyo shamba la wajomba zake.Mary Nagu!!. Kama CCM inataka kuendelea kutawala nchi hii basi waonyeshe kwamba wanajali michezo, vyanzo vya maji na misitu yetu ambayo ndiyo rasilimali pekee ambazo tunamiliki.
4). Pia inawezekana vipi mbunge/Waziri kuagiza Diwani wa kata ya Nangwa akamatwe sambamba na mimi mwanaharakati (Wilhelm Gidabuday), kwa kupigania viwanja vya watoto wetu na vyanzo vya maji ya watanzania? Polisi hawakuanza leo mauaji ya wazalendo; Tarehe 1 October, 2011, mimi Gidabuday nilisakwa usiku na mchana ili nipigwe risasi kwa ushirikiano wa Polisi wa Katesh kwa maagizo ya Mbunge, OCD na OCCID.
Nilisaidiwa na ofisa moja wa Polisi kwa yeye kunipa habari za kiintelejensia kuwa, “order imeshatolewa kuwa Diwani atakamatwa na wewe utapigwa risasi halafu wangesema walinifananisha na jambazi waliyekwa wakimtafuta siku nyingi”
!!. Mimi nikatoroka lakini Laptop yangu ilichukuliwa ili ushahidi wa picha za bonde hilo lipotezwe; mimi kwa hisia zangu
binafsi nlikuwa nimehifadhi kumbukumbu yangu katika flash.
HIVYO USHAHIDI WOTE NINAO NA NILISHAWAHI KUFIKISHA KTK VYOMBO FULANI VYA HABARILAKINI SIJUI NI KWA NINI HAWAKUWA WAZALENDO WA KUUELEZA UMMA UNYAMA HUO!!.
5). Ushahidi wa Video Clips, picha ya kawaida na documents ninao na ikihitajika sasa yoyote nitatoa, ila leo napenda kutoa USHAHIDI WA UHARIBIFU ULIOKINGIWA KIFUA NA MBUNGE WA HANANG (Ilani iliyoharibiwa na kutupwa).
Matukio muhimu yalitokea kuhusiana na ubabe huo ndani ya hifadhi ya vyanzo vya maji:
-TAREHE 28/12/2010 DC WA HANANG ALIPOKEA BARUA YANGU ILIYOKUWA NA DETAILS ZOTE (nakala ipo).
- TAREHE 06/01/2011 DC HANANG ALIKUJA KUJIONEA UHARIBIFU NA KUONYESHA MASIKITIKO MAKUBWA.
- TAREHE 04/02/2011 DC HANANG ALIHUDHURIA MKUTANO BONDENI NA KUTOA AMRI YA KILIMO KUKOMA MARA MOJA.
- TAREHE 13/03/2011 ILANI YA SEREKALI ILIWEKWA BONDENI NA HIFADHI (W) WAKIWEMO POLISI KATESH.
- TAREHE 12/04/2011 AFISA MISITU MKOA ALIKUJA AKIONGOZANA NA WAVAMIZI.
- TAREHE 14/07/2011 MKUU WA MISITU KANDA ALITEMBELEA BONDE NAKUSHAURI VIKALI KILIMO KIKOME PALE.
- TAREHE 19/07/2011 WAVAMIZI WALIN'GOA ILANI MBILI ZA SEREKALI NA KUZITUPA
- TAREHE 20/07/2011 WAVAMIZI WALIKAMATWA KWA MSAADA WA AFISA HIFADHI HANANG (Waliachiwa hadi leo).
- TAREHE 01/10/2011 NILIFANYIWA "ASSASSINATION ATTEMPT" SABABU NDIYE MSEMAJI MKUBWA WA JAMII YANGU. HATA HIVYO SIKU HIYO M/KITI WA KIJIJI ALIKAMATWA KWA SHINIKIZO LA KUNDI HILO LA WAVAMIZI NA WAFAIDIKA WA HONGO ILI KUSHINIKIZA UOGA WATU TUSIENDELEE KUPIGANIA VYANZO HIVYO VYA MAJI. KINACHOSIKITISHA ZAIDI NI MAOFISA HUSIKA KUTOJALI WAKATI WAMEAJIRIWA KUTETEA MASLAHI YA TAIFA!!.
(tunaahidi kupambana zaidi hadi kieleweke).
NB: Mary Nagu ni ndugu na rafiki muhimu sana wa wazazi wangu wapendwa, ndiye aliyemsaidia mama yangu wakati mimi na wadogo zangu tunazaliwa; lakini kwa hili sintaacha kusema ukweli kwani tukioneana aibu hatutafika!!.
No comments:
Post a Comment