MWENYEKITI wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, ameshinda kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili.
Inadaiwa kuwa Oktoba 21 mwaka jana katika maeneo ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Ilala, jijini Dar es Salaam Mchungaji Mtikila alitoa maneno ya uchochezi, dharau na kujenga chuki dhidi ya Serikali na Rais.
Akizungumza na mtandao huu baada ya kushinda kesi hiyo, Mtikila amesema "Ushindi huu niliutarajia maana hata asubuhi kabla ya kuja mahakamani niliongea na Yesu na sasa amenijibu".
Mara baada ya kushinda kesi hiyo lilizuka timbwili lingine baada ya mtu mmoja kujitokeza akiwa na RB (Report Book) akimtuhumu Mchungaji Mtikila kuwa alimtishia kumuua na ni mwizi wa viwanja. Baada ya kutaka kukamatwa na polisi mmoja aliyekuwa na cheo cha Koplo, Mchungaji alikataa kwa madai kuwa yeye ni kiongozi wa kitaifa hivyo hawezi kukamatwa na polisi mwenye cheo cha Koplo, labda polisi mwenye cheo cha SSP (Senior Superintendent of Police). Kwa kauli hiyo polisi alishindwa kumtia nguvuni.
MWENYEKITI wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, leo ameshinda hukumu ya kesi yake iliyokuwa inamkabili. Mtikila ameshinda katika kesi hiyo iliyokuwa ikisikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Elivin Mgeta. Mtikila alikuwa anakabiliwa na tuhuma za uchochezi dhidi ya serikali na kukutwa na nyaraka za uchochozi.
(PICHA ZOTE NA HARUNI SANCHAWA / GPL)
(PICHA ZOTE NA HARUNI SANCHAWA / GPL)
No comments:
Post a Comment