Jana, Jumatatu, Septemba 24, 2012 --- WANAFUNZI wa shule ya sekondari ya vipaji maalumu Ilboru mkoani Arusha wameandamana hadi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Magesa Mulongo, kushinikiza kuondolewa mkuu wao wa shule.
Akizungumza mmoja wa wanafunzi hao, ambaye ni Katibu Mkuu serikali ya wanafunzi, Ally Simalenga, alimshutumu mkuu wa shule, Jovinus Mutabuzi kuwa anawanyanyasa, “Sisi tumekuwa na maandamano kila siku, kwa sababu tunataka huyu mwalimu aondolewe kwa kuwa ameshindwa kutusaidia zaidi ya kuendeleza fitina kwa walimu wenzake na kusababisha wahamishwe,” alisema.
Wanafunzi hao wamedai wana kero nyingi zikiwemo za maeneo ya kuabudia ambayo wanadai mwalimu huyo kayafungia.Wanadai mwaka jana walilazimika kufanya maandamano na akafungua isipokuwa kwa waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ambao hadi sasa hawajafunguliwa pa kusalia.Kero nyingine walilalamikia kitendo cha kuwachangisha fedha Shilingi 190,000 wanapochelewa kuripoti shuleni wakati wa likizo na fedha hizo huzitoa bila kupatiwa stakabadhi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, baada ya kuwasikiliza kwa dakika chache, aliamuru askari kuwaondoa eneo hilo kwa ahadi kuwa serikali itafuatilia.Hata hivyo, waligoma hali ambayo Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi, Mkoa wa Arusha, Peter Mvula aliingilia kati na kuwaomba waondoke wakakubali.
via HabariLeo
No comments:
Post a Comment