Stori: Gladness Mallya na Hamida Hassan
NDOA ya msanii wa filamu ambaye pia prodyuza, William Mtitu imeacha aibu kwa baadhi ya mastaa kuingia mitini na fedha za michango waliyoahidi, Risasi Jumamosi lina fulu mkanda.
Chanzo makini kililiambia gazeti hili juzi Alhamisi kuwa mastaa hao waliahidi kuchangia fedha lakini hawakutekeleza ahadi zao na mbaya zaidi hawakutoa sababu licha ya kwamba mara kwa mara walikuwa wakikumbushwa.
“Yaani nimewashangaa sana hawa mastaa, kwa sababu waliahidi fedha lakini hawakutoa hata senti, tena wengine ni wale wanaojifanya wao ndiyo mapedeshee wa mjini, mbaya zaidi walikuwa wakizima simu zao,” kilisema chanzo.
Chanzo kiliwataja mastaa hao kwa majina kuwa ni Wema Sepetu, Flora Mvungi, Wasiwasi, Kalaghe, mtangazaji mmoja maarufu na Nice Mohamed ‘Mtunisi’.
WEMA
Mwanadada huyu kwa moyo mmoja aliahidi kutoa shilingi laki tano (500,000) lakini aliingia mitini. Alipotafutwa kwa njia ya simu na watu wa kikao cha harusi alikuwa hapatikani.
Wema alipotafutwa na paparazi wetu kwa njia ya simu ya kiganjani, iliita bila mafanikio ambapo pia alitumiwa ujumbe mfupi wa maneno (SMS) lakini hakujibu kitu mpaka gazeti hili linakwenda mitamboni.
FLORA MVUNGI
Msanii huyu naye aliahidi shilingi laki tano, hata hivyo, hakutoa chochote.
Alipotafutwa na kuulizwa, alikiri lakini akasema kuwa mama yake mzazi anasumbuliwa na moyo hivyo familia ilikuwa na mchango kwa ajili ya kumpeleka mgonjwa huyo Hospitali ya Indrapratha Apolo iliyopo jijini New Delhi, India ambapo anaendelea na matibabu.
“Jamani sikudhamiria kutotoa mchango kwa kaka Mtitu, ila nilikuwa na matatizo makubwa, mama yangu mzazi ana matatizo ya moyo, ikabidi familia iingie kwenye kuchangishana fedha ili apelekwe kwenye Hospitali ya Indrapratha Apolo, India, mpaka sasa yuko kule anapata matibabu,” alisema Flora ambaye anaishi kinyumba na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Hamis Baba ‘H.Baba’.
WASIWASI
Huyu jamaa aliahidi kuchangia shilingi laki mbili (200,000) kwenye harusi ya Mtitu lakini hakutoa na hakuweka wazi sababu ya kushindwa kwake kutimiza.
Wasiwasi alitafutwa kwa simu ili ajibu tuhuma hizo lakini simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
KALAGE
Huyu ni mjumbe aliyeahidi kwa mbwembe zote kwamba, piga ua galagaza, lazima harusi ya Mtitu ambaye ni besti yake, achangie shilingi laki mbili, lakini naye kama Wasiwasi, aliingia mitini.
Mpaka tunakwenda mitamboni, simu yake ya mkononi haikuwa hewani.
MTANGAZAJI MAARUFU
Mtangazaji maarufu ambaye awali alikuwa kituo kimoja cha redio cha jijini Dar es Salaam alikovuma sana, baadaye akahamia kituo kingine akipiga mzigo hadi sasa, naye aliingia mitini.
Jamaa hakujikweza sana, alihidi ‘kulala ubavu’ na kutoa shilingi laki moja tu (100,000), lakini hakufanya hivyo, akaunga mnyororo wa Wema na wengine katika kuingia mitini hadi siku ya harusi bila kutoa sababu.
Alipotafutwa kwa njia ya simu Alhamisi iliyopita kwa lengo la kueleza sababu za kuingia mitini, simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
MTUNISI
Msanii huyu wa filamu aliahidi kuunonesha mfuko wa mchango wa harusi kwa kutoa shilingi laki moja lakini hakutoa. Alipotafutwa na mapaparazi wetu, hakupatikana hewani.
Hata hivyo, wapo baadhi ya mastaa walioahidi kiasi kidogo lakini wakatoa kikubwa.
JACQUELINE WOLPER
Yeye aliahidi kutoa shilingi laki mbili lakini mpaka mwisho alitumbukiza shilingi laki nne (400,000) na hivyo kufidia mapengo ya mastaa wenzake ‘waliozama baharini’.
IRENE UWOYA
Huyu mdada aliahidi kutoa shilingi milioni moja (1,000,000) lakini kuna siku alisikia bajeti ya ukumbi inagoma, akaahidi kuongeza shilingi laki nne na akatimiza ahadi tena akiwa nje ya nchi.
“Tunamshukuru sana Uwoya, aliahidi milioni, baadaye bajeti ya ukumbi ilipokaa vibaya, akasema ataongeza laki nne, akatuma akiwa nje ya nchi, kwa kweli alisaidia sana, si ajabu harusi ingeishia kwenye ndoa tu kanisani,” alisema mmoja wa wanakamati wa harusi hiyo.
Kwa upande mwingine, pongezi zilishushwa kwa wasanii walioonesha moyo wa kuchangia, hasa Katibu wa Kamati, Herieth Chumila na Mtunza Hazina, Mama Rolaa.
Ndoa ya Mtitu ilifungwa Septemba 8, mwaka huu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Posta jijini Dar na kufuatiwa na sherehe iliyofanyika katika Ukumbi wa Urafiki, Ubungo, Dar
No comments:
Post a Comment