EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, September 15, 2012

Taarifa ya Naibu Waziri kuhusu mtihani wa kumaliza elimu ya Msingi, 2012


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI MWAKA 2012

 Ndugu wananchi,

Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi Tanzania Bara utafanyika tarehe 19 na 20 Septemba, 2012.  Jumla ya wanafunzi 894,881 wamesajiliwa  kufanya mtihani huo ambapo   wavulana ni  426,285 sawa na asilimia 47.64  na wasichana ni 468,596  sawa na asilimia 52.36. Aidha, kati ya  wanafunzi hao, wapo wanafunzi 874,379  watakaofanya mtihani huo kwa lugha ya Kiswahili na wanafunzi 20,502 watafanya kwa lugha ya Kiingereza ambayo ndiyo waliyoitumia kujifunzia.  Wanafunzi wasioona waliosajiliwa kufanya mtihani ni 92 wakiwemo wavulana 53 na wasichana 39.  Watahiniwa wenye uono hafifu ambao huhitaji maandishi makubwa ni 495, kati yao wavulana ni 238 na wasichana ni 257.

Mtihani huu utafanyika kwa mara ya kwanza kwa kutumia teknolojia mpya ya ‘Optical Mark Reader’ (OMR), ambapo watahiniwa watatumia fomu maalum za OMR kujibia mtihani na majibu yao yatasahihishwa kwa kutumia kompyuta.  Masomo yatakayotahiniwa katika mtihani huo ni Kiswahili, English Language, Sayansi, Hisabati na Maarifa ya Jamii. 

Ndugu wananchi,

Maandalizi yote kwa ajili ya mtihani huo yamekamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa karatasi za mitihani, kusambazwa kwa fomu maalum za   kujibia mtihani na nyaraka zote zinazohusu mtihani huo. Mafunzo maalum kwa ajili ya matumizi ya fomu za OMR yamefanyika kwa lengo la kuwaandaa watahiniwa, wasimamizi pamoja na viongozi wa elimu katika ngazi mbalimbali ili waweze kutumia ipasavyo teknolojia hiyo. 

Ndugu wananchi,

Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi ni muhimu kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla kwa kuwa unahitimisha ngazi ya Elimu ya Msingi na kufungua milango kwa ajili ya elimu ya sekondari.  Hivyo, matokeo ya mtihani huu hutumika katika uchaguzi wa wanafunzi wanaojiunga na Elimu ya Sekondari.   Kwa kuzingatia umuhimu wa mtihani huo, napenda kutumia fursa hii kutoa wito kwa Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha kuwa taratibu zote za mitihani zinazingatiwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa  mazingira yanakuwa salama na tulivu na kuzuia mianya yote inayoweza kusababisha udanganyifu.

Napenda pia kutoa wito kwa wasimamizi wa mitihani kufanya kazi yao ya kusimamia kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu.  Wapo baadhi ya wasimamizi ambao wamekuwa wakishiriki katika kuwasaidia watahiniwa kufanya udanganyifu kwenye mitihani.   Napenda kuwaasa tena wasimamizi kujiepusha na vitendo hivyo vya udanganyifu kwani serikali haitasita kuchukulia hatua kali za kisheria kwa yeyote atakayebainika kukiuka taratibu za mitihani.

Kwa upande wa wanafunzi watakaofanya mtihani mwaka huu, ninaamini kuwa walimu wamewaandaa vizuri katika kipindi chote cha miaka saba ya Elimu ya Msingi.  Hivyo, ni matarajio yangu kuwa mtaufanya mtihani huo kwa utulivu na kuzingatia taratibu zote za mitihani ili matokeo ya mtihani yaoneshe uwezo wenu halisi kulingana na maarifa na ujuzi mliopata katika Elimu ya Msingi.  Serikali inawaasa wanafunzi wote kutojihusisha na vitendo vyovyote vya udanganyifu katika mtihani kwani watakaobainika watafutiwa matokeo yao yote ya mtihani. 

Ndugu wananchi,

Natoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano unaotakiwa katika kuhakikisha kwamba mtihani huo  unafanyika kwa amani na utulivu wa kutosha bila usumbufu unaoweza kusababishwa na shughuli za kijamii hasa katika maeneo ya jirani na shule.

Mwisho, napenda kuwaasa tena wanafunzi, walimu na wananchi wote kwa ujumla kujiepusha na vitendo vya udanganyifu wa aina yoyote katika Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi. Nawaomba pia raia wema wasisite kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapoona au kuhisi mtu au kikundi cha watu kinajihusisha na udanganyifu wa aina yoyote katika mtihani huo.

Nawatakia watahiniwa wote heri na fanaka katika mtihani utakaofanyika tarehe 19 na 20 Septemba, 2012.

MHESHIMIWA PHILIPO AUGUSTINO MULUGO (MB) 
NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

15 SEPTEMBA, 2012


No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate