EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, September 20, 2012

SPIKA WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI AMTEMBELEA RAIS KIKWETE IKULU, DAR ES SALAAM


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea nakala ya machapisho mbalimbali ya Bunge la Afrika Mashariki toka kwa Spika wa Bunge hilo Bi. Margaret Banbtonbg Zziwa alipomtembelea Ikulu Jumatano Septemba 19, 2012.
(PICHA NA IKULU)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amelishauri Bunge la Afrika Mashariki (EAC) kuzingatia na kufuata maelekezo yaliyomo kwenye Mkataba ulioanzisha Jumuiya hiyo wakati wa kuwasilisha na kujadili hoja zao.
Rais Kikwete ametoa ushauri huo jana jioni (19 Septemba, 2012) alipokutana na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mheshimiwa Margareth Ziwa, Ikulu.
“Jumuiya ya Afrika Mashariki inahusika na masulala yaliyomo kwenye Mkataba (Treaty) na Itifaki zilizoanzisha Jumuiya hii na kila nchi inawajibu wa kuzingatia kilichomo kwenye Mkataba” ameeleza na kufafanua “Lakini pia msisahau kuwa hizi ni nchi huru zenye sheria na taratibu zake ambazo nchi zinapaswa kuzifuata na kuzizingatia, hivyo Bunge la Afrika Mashariki linaweza tu kuzishauri lakini sio kuzielekeza au kuzilazimisha kutekeleza jambo ambalo halimo kwenye Mkataba ambao nchi hizi zimetiliana saini” ameongeza.
Mheshimiwa Ziwa amefika Ikulu kujitambulisha kwa Mheshimiwa Rais baada ya kushika wadhifa huo hivi karibuni.
Mheshimiwa Ziwa ni raia wa Uganda na ni Mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo inajumuisha nchi za Burundi, Kenya, Rwanda, Uganda na Tanzania.
Rais amewataka wabunge wapya kusoma Mkataba na Itifaki  zilizoanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki ili waweze kutekeleza majukumu yao vizuri bila kuingilia uhuru na taratibu za nchi wanachama.
“Jipeni muda wa kutosha wa kusoma na kuzielewa taratibu za Mkataba na Itifaki iliyoanzisha Jumuiya hii, hii itawasaidia sana katika kujenga hoja zenu na jinsi ya kuziwasilisha” amewakumbusha kuwa hiyo ndiyo njia pekee ambayo itawafanya kutekeleza kazi na wajibu wao kwa umakini na uangalifu bila kuingilia taratibu za mabunge ya nchi wanachama.
Wakati huo huo, leo asubuhi  (20 Septemba, 2012) Rais amekutana na Katibu Mkuu wa EAC  Dkt. Richard Sezibera ambaye amefika kumueleza Rais juu ya maendeleo na ratiba  ya shughuli muhimu za Jumuiya hiyo ambazo EAC inatarajia kuzifanya kabla ya mwisho wa Mwaka.
Rais amempongeza Dkt. Sezibera kwa maendeleo ya Jumuiya hiyo na jinsi shughuli za utekelezaji zinavyokwenda kulingana na ratiba ya EAC.
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu.
Dar-Es-Salaam
20 Septemba, 2012

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate