Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande ameahirisha kesi ya rufaa ya aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini, hadi Oktoba 2, 2012 kwa mujibu wa maombi ya mawakili wa pande zote mbili, CCM na CHADEMA walioandika barua ya kuomba kuahirishwa kwa kesi hiyo baada ya kifo cha mzazi wao ambaye maziko yake yanatarajiwa kufanyika Septemba 22, 2012.Jaji Mkuu ametoa amri fupi ya Mahakama kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye alikuwa anajibu maombi wa pili aunganishwe kama mtu muhimu katika kesi hiyo.Kesi hiyo ambayo imesikilizwa kwa takribani saa mbili chini ya Jaji Mkuu na Majaji wengine wawili wa Rufani, ni ya kukata rufaa kupinga kuvuliwa ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA).
Tundu Lissu, anamtetea Lema na kaka yake, Alute Mughwai, anawatetea walalamikaji.Wakili Mughwai anashirikiana na wakili Modest Akida kuwawakilisha wadaiwa kwenye shauri hilo ambao ni wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo, waliofungua shauri lililotengua ubunge wa Lema wakidai kuwa wakati wa kampeni alimdhalilisha mgombea wa CCM, Dkt. Batilda Burian kwa kutumia lugha za matusi.Awali, Lema kupitia wakili wake, Method Kimomogoro, anayesaidiana na Lissu, aliwasilisha kwenye mahakama hiyo hoja 18 za madai akipinga kutenguliwa kwa ubunge wake na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili 5, mwaka huu.
Kwenye baadhi ya madai hayo, Lema aliiomba Mahakama ya Rufaa kutengua uamuzi wa Mahakama Kuu, uliotengua ubunge wake, huku akiitaka imtangaze kuwa mbunge halali wa Jimbo la Arusha Mjini.Aidha, aliitaka mahakama hiyo ya juu, iwaamuru walalamikiwa katika shauri hilo walipe gharama za rufaa hiyo pamoja na zile za kesi iliyomalizika kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.Katika madai mengine, Lema anamlalamikia Jaji Gabriel Rwakibarila, aliyesikiliza kesi hiyo kuwa alitoa uamuzi wake kwa kuzingatia maneno ya uvumi, huku akipuuza ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.Lema anadai kuwa jaji alikosea wakati alipoamua kuwa mpiga kura yeyote anaruhusiwa kupinga matokeo ya uchaguzi hata kama haki zake za msingi hazijaguswa.
No comments:
Post a Comment