EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, September 11, 2012

WAZIRI NCHIMBI ATIMULIWA MAANDAMANO YA WAANDISHI WA HABARI KUPINGA MAUAJI YA DAVID MWANGOSI

Mhariri Mkuu wa NIPASHE, Jesse Kwayu akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari kufuatia maandamano ya kupinga mauaji ya David Mwangosi (katika picha kulia) kwenye viwanja vya Jangawani, jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo.  
Waandishi wa habari wakiandamana kuelekea kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo.


Waandishi wa habari wakiandamana kuelekea kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo.

Waandishi wa habari wakiandamana kuelekea kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo.
Mojawapo ya mabango yaliyokuwapo kwenye maanamano ya waandishi wa habari ya kupinga mauaji ya mwandishi mwenzao kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo.

Waandishi wakisapoti jambo wakati wa mkutano wao baada ya maandamano ya kupinga mauaji ya David Mwangosi asubuhi ya leo
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi, amekumbana na fadhaa ambayo haikutarajia wakati alipotimuliwa katika maandamano ya waandishi wa habari ya kupinga mauaji ya mwandishi mwenzao wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, David Mwangosi, wakati alipozuka bila mwaliko.

Huku wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe tofauti, waandishi waliandamana kuanzia kwenye ofisi za Channel Ten katikati ya jiji la Dar es Salaam na kutembea hadi katika viwanja vya Jangawani lakini walipofika mwisho wa maandamano yao walipigwa na butwaa baada ya kumkuta Waziri Nchimbi akiwa wa kwanza kufika katika eneo hilo tayari kupokea maandamano.

Wakati Nchimbi akijiandaa kuanza kuzungumza mbele ya wanahabari, upinzani mkali ukazuka kwa waandishi dhidi ya kiongozi huyo wa serikali wakitaka aondoke mahala hapo kwani maandamano hayo yalikuwa hayamuhusu.

"Atokee.... aondokee.... hatumtakiiii.... nani kamleta hapa?" yalikuwa ni baadhi ya maneo yaliyokuwa wakitolewa kwa sauti kubwa kupinga uwapo wa waziri Nchimbi mahala hapo.

Huku akizomewa, Waziri Nchimbi alijaribu kuvumilia aibu hiyo kwa takriban dakika tano huku pengine akitumai kwamba watamruhusu kuzungumza kilichompeleka mahala hapo.

Mwandishi wa habari mkongwe, ambaye pia ni mwanasheria, Nyaronyo Kicheere, alisogea mbele ya umati wa waandishi na kusimama jirani na alipokuwapo waziri Nchimbi na kusema: "Tumeambiwa tunakuja hapa kwa ajili ya mkutano wa waandishi wa habari na utapokewa na jukwaa la wahariri, inakuwaje tupokewe na mtu mwingine. Hatumhitaji mtu mwingine hapa, aondoke."

Baada ya kauli hiyo, waziri Nchimbi aliondoka mahala hapo na kuzua shangwe kubwa kwa waandishi ambao pia walimsindikiza kwa kumzomea mpaka alipoingia katika gari lake la wizara. Hakuja na gari lake la waziri.

Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari walizungumza na kukemea mauaji hayo na bila ya kuuma-uma maneno walisema kwamba Mwangosi aliuawa kwa kulipuliwa na polisi na kwamba waliohusika wote wachukuliwe hatua za kisheria.

"Waandishi na wafanyakazi wengine wanalipa kodi ilipolisi wapate magwanda, wapate bunduki, wapate mabuti na wanalipwa ili walinde raia na sio kuua raia, vitendo kama hivi havikubaliki," alisema Jesse Kwayu, mhariri mkuu wa gazeti la NIPASHE.

Mwandishi mkongwe, Masoud Sanani, aliongeza: "Waarabu wanasema 'wal kiswaswa haq' yaani 'kisasi ni haki', lakini sisi kwa busara tunasema kwamba hatuna kisasi ila tunataka mambo haya yawe mwisho, waandishi waachwe wafanye kazi zao kama askari wanavyoachwa wafanye kazi zao."

"Tumeshasikia askari akitingishwa kidogo, mtu anashitakiwa kwa kumzuia askari kufanya kazi yake, tunataka waandishi nao waachwe wafanye kazi yao," alisema.

Waandishi walitaka familia ya marehemu Mwangosi ilelewe na watoto wasomeshwe mpaka watakapofikia.

Miongoni mwa mabango yaliyokuwapo katika maandamano hayo yalisomeka: "Bunduki na mabomu hayatazuia kalamu zetu kuandika ukweli," "Hatuogopi vitu vizito wala vitu vya ncha kali".... 

Yalikuwa ni maandamano ya amani. Hapakuwa na vurugu zozote na askari waliokuwapo wengi walikuwa mikono mitupu bila ya silaha yoyote hata virungu ukiacha wachache waliobeba silaha na askari wa usalama barabarani waliongoza maandamano wakizuia magari wakati waandishi wakipita katika njia zote kuelekea kwenye viwanja vya Jangawani.
                         chanzo cha habaristraikamkali.blogspot.com

1 comment:

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate