Hakika
si kila ajali itokeayo barabarani husikitisha bali zipo ambazo pindi
zinapotokea watu hufurahi na kustaajabu vile ajali ilivyotokea. Hivi
ndivyo ilivyolikumba gari hilo dogo Toyota Spacio T 629BRL iliyokuwa
ikitokea maeneo ya Uwanja wa Ndege kuelekea mjinui na kupinduliwa kama
inavyoonekana katika picha katika barabara ya Nyerere karibu na kituo
cha Tazara jijini Dar es Salaam jana alasiri.
Mashuhuda
wa ajali hii wanapasha kuwa waluiona kama mchezo wa sinema gari hii
ilivyokuwa ikipinduka kiasi hata dereva wake kuto kutambua na kushtuka
gari ipo chali. Mashuhuda hao wanap[asha kuwa chanzo ni kuopigwa pasi na
lori la mizigo.
Wanadai
kuwa baada ya kupigwa pasi gari hilo dogo lilinasa katika ngao ya lori
hilo na taratibu wakati yanaenda katika foleni basi walishtukia gari
ikigeuzwa ilikotokea na mara wakashangaa matairi yapo hewani.
Polisi
usalama barabarani walifika na kuchukua maelezo ya ajali na kisha
kuomba wenuyenguvu walinyanyue gari hilo ili kuepusha msongamano
barabarani.
Walijitokeza watu na kulinyanyua gari hilo ambalo liliharibika vibatya upande mmoja ambao ulipigwa pasi kisha kuruka sarakasi.
No comments:
Post a Comment