MSANII maarufu wa filamu za
maigizo nchini, Mwanaidi Suka ‘Mainda’ ameporomoshewa tuhuma nzito za
kuitibua ndoa ya mganga wa kienyeji, Ratif Mkonga ‘Dokta Keita’, mkazi
wa Kigogo Luhanga, jijini Dar es Salaam.
Stori: Richard bukos
Mwanaidi Suka ‘Mainda’
Chanzo cha habari kilicho karibu na sangoma huyo, kilidai kuwa ndoa
ya mganga huyo ilianza kutibuka tangu mwanzoni mwa mwaka huu baada ya
wapambe nuksi kumpasha habari mkewe, Rehema Nassoro kuwa mumewe
anabanjuka na Mainda.
Kufuatia henyahenya hilo, ilifikia wakati Rehema aliondoka nyumbani
hapo akidai anamuachia nyumba Mainda huku akitishia kuwa atakachomfanyia
msanii huyo atakijua mwenyewe. Hata hivyo, waungwana waliingilia kati
na kumtuliza alee familia.
Baada ya kupata taarifa hizo, paparazi wetu alivamia kilinge cha sangoma huyo na kumkuta akimbembeleza ‘waifu’ wake ili mambo yaishe.Baada ya kuhojiwa na paparazi juu ya sakata hilo, Keita alisema mkewe alipewa uzushi huo na wapambe nuksi kuwa anabanjuka na msanii huyo, jambo ambalo alidai si la kweli.
Baada ya kupata taarifa hizo, paparazi wetu alivamia kilinge cha sangoma huyo na kumkuta akimbembeleza ‘waifu’ wake ili mambo yaishe.Baada ya kuhojiwa na paparazi juu ya sakata hilo, Keita alisema mkewe alipewa uzushi huo na wapambe nuksi kuwa anabanjuka na msanii huyo, jambo ambalo alidai si la kweli.
Keita aliendelea kuweka wazi kuwa Mainda ambaye kwa sasa anajulikana pia kwa jina la Ruth ni mtu wake wa karibu na siku moja alikuwa naye kwenye Ufukwe wa Coco, Dar wakipunga upepo na kusema kuwa huenda kuna mpambe aliwaona na kumpelekea mkewe taarifa za uchonganishi.
Aliongeza kuwa staa huyo wa filamu, anafahamiana pia na mkewe na
amewahi kwenda nyumbani kwake mara kadhaa hivyo yeye kuonekana naye
sehemu wakipunga upepo si skendo.
Baada ya kumsikia sangoma huyo, paparazi wetu alimgeukia mkewe ambaye
naye alikiri kuwa taarifa hizo alitonywa na mtu wake wa karibu ambaye
alikataa kumtaja na kueleza kuwa aliumia sana kugundua kuwa, kumbe staa
huyo anamzunguka.Baada ya hapo, mwandishi wetu alimtafuta Mainda mpaka nyumbani kwake,
Kijitonyama, Dar bila mafanikio na alipomkosa, aliamua kumpigia simu.
Alipopatikana hewani na kusomewa mashitaka yake, Mainda alisema:
“Mimi sijawahi kwenda kupunga upepo kwenye ufukwe wowote wenye mchanga, kama ni kupumzika labda fukwe za ukweli lakini siyo hapo Coco, huyo mwanaume unayemsema mi wala simjui, ‘plizi’ niache nilale nimechoka.“Aaah! Coco, sasa nimekumbuka, kuna siku moja nilikuwa na akina Steve Nyerere (msanii) tulikuwa tunashuti filamu lakini simkumbuki huyo mwanaume.
No comments:
Post a Comment