EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, October 16, 2012

Askofu Mkuu wa Kanisa la TAG atoa tamko kuhusu choko choko za udini.

Oktoba 12 mwaka huu, matukio mabaya na yenye kutia doa sifa ya amani umoja na Utengemano wa Taifa la Tanzania, yalijitokeza huko Mbagala Jijini Dar es Salaam, wakati watu wenye jazba wanaoaminika kuwa ni Waislamu wenye msimamo mkali walipovamia makanisa saba ...na kuyachoma moto eti kwa kulipiza kisasi cha mtoto aliyekojolea kuran katika utani wa kitoto.
Katika mkasa huo ambao ni kama muendelezo wa ghasia zingine zilizotokea kule Zanzibar miezi michache iliyopita na kuteketeza makanisa mbalimbali mbali na kuharibu mali za kanisa na zile za watu binafsi.
Tukio la Mbagala limesababisha makanisa saba kuharibiwa vibaya, mali kuibiwa na hata kuhatarisha maisha ya watanzania na kuwafanya waishi kwa hofu na kupoteza matumaini.
CHANZO CHA TUKIO
Kwa mujibu wa walioshuhudia, Polisi na wahusika (Waislamu) chanzo cha ghasia hizo na mabishano ya kitoto baina ya watoto wa dini ya Kiislamu na kikristo, waliobishana kuwa ikiwa mtu atakojolea kuran na kuitemea mate atageuka mbuzi au nyoka.
Lakini baada ya tukio hilo la kitoto watu walilikuza na kulipeleka kwenye misikiti na hivyo kuchocheza ghasia. Kimsingi tukio lenyewe ni jepesi sana ukilinganisha na matokeo yake. Ukweli kwamba waliofanya utani huo ni watoto na chanzo chake ni mabishano ya kitoto, unatia shaka kuwa huenda kuna hoja nyuma ya pazia ambayo isipotazamwa kwa makini inaweza kulete matokeo mabaya sana.
Jambo linalonitia shaka ni kufanana kwa matukio ya kuchomwa moto kwa makanisa ya Zanziabar na ya Mbagala ambapo hakukuwa na uhusiano wa vyanzo vya ghasia na makanisa husika.
Mfano; Ghasia za Zanzibar zilizopelekea kuangamizwa kwa makanisa zinaelezwa kuwa zilitokana na kikundi cha Kiislamu cha Uamsho wa Mihadhara, kilichokuwa kikiandamana kudai mjadala wa Muungano, lakini zikaishia kwenye uchomaji wa makanisa, hapa hauonekani uhusiano wa kanisa na Muungano; nalazimika kujiuliza kulikoni?
Vivyo hivyo tukio la Mbagala halina uhusiano wa moja kwa moja na kanisa kwa kuwa hakuna ushahidi wala hata tetesi kuwa mtoto huyo alitumwa na kanisa lolote. Wahusika wa dini ya Kiislamu akiwepo Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, analielezea tukio la kitoto kama lisilostahili hata mtu kufunguliwa mashtaka bali kuelekezwa tu. Ni vipi lisababishe uchomaji wa makanisa?

MAKANISA YALIYOCHOMWA MOTO
Katika ghasia hizo za aina yake, makanisa saba yamethibitishwa kuharibiwa kwa kuchomwa moto, kupasuliwa vioo, viti na kuibiwa vyombo vya muziki na jenereta. Makanisa hayo ni TAG Kizuiani, Agape, Kibonde maji, SDA Sabato, Mbagala Kizuiani, Katoliki Kristo Mfalme Mbagala Rangi Tatu, Anglican Mbagala Kizuiani, KKKT, Mbagala Zakhem na TAG, Shimo la Mchanga.
Pamoja na majengo hayo kubomolewa kwa viwango tofauti mengine yakichomwa moto, pia wahusika waliiba Genereta, na vyombo vya muziki vya makanisa hayo na kuvunja magari na baadhi yao kuchomwa moto.
Choko choko zilizinazoweza kuwa chanzo cha matukio hayo ni:
Januari sita mwaka huu, kikundi kimoja kinachoitwa JUAKITA, kiliitisha kongamano la kujadili katiba mpya Tanzania, kwa upande wa Waislamu. Katika kongamano hilo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam kulitolewas kauli za kichozi kama:
1. Lazima Rais ajaye atoke Zanzibar
2. Kukabiliana na ukuaji wa kasi wa dini ya Kikristo

3. Kupinga Muungano ili kuupa nguvu Uislamu
4. Kupigana kufa na kupona kutetea maslahi yao wakati huu wa kuandaa katiba mpya.

Kauli hizo zilitolewa na Sheikh Nasoro Mohamed, kutoka Zanzibar, ambaye alikuwa mgeni rasmi. Baadaye zikaandaliwa kanda za CD zilizosambaza ujumbe huo.
Uchunguzi unaonesha kuwa uchochezi huu umekuwa ukiwaandaa watu kusubiri vijitukio vidogo tu ili kulipua ghasi. Tuliona jinsi makanisa yalivyochomwa kule Zanzibar.  Kwa kuwakumbusha tu, Makanisa yaliyoangamizwa katika tukio hilo ni: EAGT, Elimu Pentecost na TAG, Anglikana, Katoliki na FPCT.

Ni jambo la kusikitisha kuwa matukio haya yanatokea siku mbili tu kabla ya maadhimisho ya miaka 13, ya kifo cha Rais wa Kwanza, Mwl. Julius kambarege Nyerere. Leo hotuba na midahalo inarindima kila mahali kumuenzi Nyerere, lakini wengi wetu tukiwa tumejaa majozi baada ya nyumba zetu za ibada kuharibiwa katika matukio yanayoashiri hatari kubwa.Hofu yangu ni kuwa, roho hii ya ubaguzi wa kidini ambayo Baba wa Taifa hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliifananisha na dhambi ya kula nyama ya mtu, imekuwa ikiyatafuna mataifa ya Afrika kama ifuatavyo:
  1. Mwaka 2000, vuguvugu la kuanzishwa kwa utawala wa Kiislamu (Sharia), lilianza kwenye majimbo ya Kaskazini mwa Nigeria, miaka michache baadaye majimbo kadhaa yakajitangazia sheria hizo na tangu wakati huo kumekuwa na mapambano yasiyoisha. Takwimu zinaonesha kuwa katika miaka ya karibuni zaidi ya Wakristo 500 wameuawa kikatili na makanisa kuchomwa moto.
  2. Roho hii imekuwa ikienea kwa kasi katika maeneo mbali mbali ya Afrika ambapo imelikumba taifa la Mali, majimbo ya kaskazini tayari yametangaza kujitenga na kuna vuguvugu lenye kuhusisha mapigano ya silaha.
  3. Itakumbukwa kuwa miezi michache tu ilizopita vuguvugu hili la kudai utawala wa kidini liliibuka nchini Kenya ambapo watu wanaojiita wanaharakati walianzisha madai ya kutaka eneo la Pwani kujitenga na Jamhuri ya Kenya na kujitangazia taifa la Kiislamu.
  4. Katika tukio hilo inasemekana mtoto huyo alitengenezewa mabishano ya kitoto kuwa akichoma kurani atakuwa chizi naye akabisha kisha akapewa kiberiti na kurani akachoma tena walioandaa mzaha huo wakamkamata na kumpeleka mahakamani.Tukio linalofanana na hilo lilitokea tena Bagamoyo mkoani Pwani ambapo mtoto wa kike alishtakiwa na hata kuhukumiwa kifungo kwa madai ya kuchoma kuran lakini tukio lilikuwa katika mabishano ya midhaha ya kitoto.

WITO WANGU

Natoa wito kwa Wakristo wote nchini kujiepusha na mizaha inayoweza kutengeneza sababu za kulipuka kwa ghasi na kutengeneza mwanya wa watu wenye nia mbaya kutekeleza agenda zao zaria Ili kulinda amani umoja na utengemano wetu, nawasihi viongozi wa makanisa kuonya na kukemea waumini na watoto wetu wasishiriki kwa namna yoyote ile mizaha inayopelekea kuchoma au kuharibu vitabu au nyaraka za kidini.
Nawasihi watanzania wote kwa ujula kujiepusha na mizaha ya kidini inayoweza kuchafua amani yetu, na pale jambo lolote lenye kukera linapotokea tujiepushe kuwa mawakala wa shetani wa kueneza chuki badala ya amani na upendo.
USHAURI WANGU KWA SERIKALI NA VIONGOZI 

Nawashauri viongozi wa Serikali ambao leo wanatoa matamko na kushiriki midahalo ya kumuenzi Mwl. Nyerere kukumbuka kuwa huyo alikuwa na mapenzi makubwa na amani na umoja wa taifa. Kwa hiyo kumuenzi kwa vitendo ni kudumisha utawala bora, unaofuata sheria usio na chembe ya ubaguzi wa aina yoyote.
Kulipuka majukwaani kumuenzi Nyerere bila kuilinda na kuitetea amani ya nchi ni kujidanganya.
Ni wajibu wa kila Mtanzania kutii sheria na mamlaka kwa kuwa zimewekwa/kuruhusiwa na Mungu, hivyo kuziasi ni Kumuasi Mungu, yaani ni dhambi. Hivyo kila Mtanzania anastahili kukumbuka wajibu wake wa kutii mamlaka.
Viongozi wenzangu wa dini wakumbuke kuwa wana wajibu mkubwa katika jamii, na jamii inawasikiliza hivyo ni vyema wakawa makini katika matamshi na maelekezo yao ili wasiwe chanzo cha kuchochea vurugu za kidini na uvunjaji wa amani.
Pia ningependa kuwashauri viongozi wa serikali kusimama imara katika kusimamia sheria na haki, na kuepuka kauli au vitendo vitakavyofanya baadhi ya watanzania kudhani kuwa hawatendewi haki.
Ni vema ieleweke kuwa matukio kama haya ya uvunjaji wa amani yasipodhibitiwa na kukomeshwa haraka yanaweza kuumba chuki ambayo inaweza kuibua mlipuko mkubwa na machungu kwa wananchi na matokeo yake yakawa mabaya kwa Taifa zima. Hekima na busara inatufundisha kuwa tusipoziba ufa tutajenga ukuta.
Ni vyema wenye dhamana ya kuongoza wakakumbuka kuwa wanawajibu mbele ya Mungu aliyewaweka au kuwaruhusu kuingia madarakani na siku moja watatoa hesabu mbele zake.
Ni vyema viongozi wa Serikali wakajizuia kufanya maamuzi yanayoashiria upendeleo kwa baadhi ya makundi ya kidini na kukiuka utawala wa sheria, mfano; kutii waandamanaji na kuwaachia bila mashrti watu waliokamatwa kwa mujibu wa sheria kuna jenga kiburi kwa makundi yenye kiu ya matumizi ya nguvu na kujenga hofu kwa pande zingine.Ni vyema mamlaka zikasiamama katika sheria na kufanya hukumu kulingana sheria badala ya kuamua mambo ya kisheria kisiasa.

WITO MAALUMU KWA VIONGOZI WA DINI

Nitumie nafasi hii kuwasihi vingozi wenzangu wa dini, kusimama imara katika kuombea taifa na kuhubiri kwa nguvu ili kukabiliana na giza la kiroho ambalo linatishia kuifunika nchi.Takwimu za karibuni kabisa za utafiti uliofanywa na taasisi ya Washnton DC iitwayo, Pew Research Centre, na kurushwa na Televisheni ya CNN, Katika kipindi chake cha Inside Africa, zilionesha kuwa watanzania asilimia 93, wanaamini mambo ya ushirikina na uchawi wakati Uganda ni asilimia 29 na Kenya ni asilimia 27 Tu. Mahali ambapo giza la kiroho limezingira kiasi hiki ni lazima matukio ya kishetani yashamiri tuchukue hatua.Mwisho, natoa wito kwa watanzania wenzangu tuulinde umoja, amani na utengamano wa taifa letu, tuikimbie dhambi ya ubaguzi kwa kuwa tukiiruhusu itatuangamiza sote. Tuliombee taifa letu na kukiwa na mbegu ya chuki tuimalize kwa njia ya majadiliano na vikao vya pamoja vinavyohusisha viongozi wa dini zote na serikali pia.

Imetolewa leo 14/10/2012

Na Dk. Barnabas Mtokambali
Askofu Mkuu wa TAG.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate